

Chanzo cha picha, Reuters
Marekani ni kawaida kwa makampuni makubwa kufadhili wanasiasa kwa kiasi kikubwa tu cha fedha
Baadhi ya wanasiasa wa Republican tayari wameanza kuhisi athari ya vurugu vya Januari 6 ambapo wafuasi wa Trump walivamia bunge.
Zaidi ya makampuni 20 ya Marekani yametangaza kusitisisha ufadhili wao kwa kampeni za chama cha Republican hasa kwa wabunge wa chama hicho waliopinga ushindi wa mgombea wa Democratic Joe Biden.
Ghasia zilitokea wakati wa kikao maalumu katika mabunge yote mawili cha kuidhinisha kura za wajumbe ambacho kilikatizwa na uvamizi wa eneo la Capitol kulikotekelezwa na wafuasi wa Trump waliozua vurugu.
Lakini baada ya kikao hicho kilichovurugwa kurejelewa tena, zaidi ya wabunge 100 wa bunge la Wawakilishi kadhaa, wengi wao wakiwa kutoka chama cha Republican ambao walikuwa wanapinga matokeo hayo, wabadilisha msimamo wao.
Chanzo cha picha, Reuters
Watu watano walifariki dunia kwasababu ya uvamizi wa bunge.
Orodha ya makampuni ambayo yameamua kusitisha ufadhili wake yanazidi kuongezeka kila siku
Chanzo cha picha, Reuters
Kampuni ya hoteli ya Marriott imesitisha ufadhili wake kwa wabunge waliopinga kuidhinishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Novemba 3
Baadhi ya kampuni hizo zimeamua kusitisha ufadhili wao wote wakati wanapitia tena sera zao kwasababu ya uvamizi wa bunge uliotokea huku wengine wakiamua kusitisha ufadhili wao hususan kwa wabunge waliopinga kuidhinishwa kwa matokeo ya kura za wajumbe.
Katika kundi la pili, haya ni makampuni ambayo ni maarufu:
- Kampuni ya kimataifa ya masuala ya fedha ya Morgan Stanley.
- Kampuni ya hoteli ya Marriott.
- Kampuni ya Dow: Kampuni hiyo ilisema kuwa hatua ya kusitisha ufadhili wake kwa chama cha Republican itatekelezwa kwa miaka miwili kwa wale wa Bunge la Wawakilishi huku bunge la Seneti ikiwa ni hadi miaka sita.
- Kampuni ya mawasiliano ya AT&T, ni mingoni mwa wafadhili wakubwa wa chama cha Republican Marekani.
- Kampuni ya General Electric imekatiza ufadhili wake hadi mwisho wa mwaka 2022. Baada ya hapo, bodi ya wafanyakazi ambayo inahusika na ufadhili huo itapitia tena sera yao pamoja na, “kesi moja baada ya nyingine” maombi ya ufadhili kutoka kwa wabunge waliopinga kuidhinishwa kwa matokeo ya kura za wajumbe zilizomuidhinisha Biden kama mshindi.
- Kampuni ya kadi ya Hallmark: Kampuni hiyo yenye makao yake Kansas iliongeza kwamba inataka kurejeshewa pesa ilizotoa kwa wabunge wa Republican Seneta Josh Hawley (Missouri) na Roger Marshall (Kansas). “Hallmark inaamini kuwa ubadilishanaji wa madaraka ndio msingi wa mfumo wetu wa demokrasia na ndio sababu tunachukia aina yoyote ile ya ghasia,” kampuni hiyo ilielezea katika taarifa. “vitendo vya hivi karibuni vya Seneta Josh Hawley na Roger Marshall haviwakilishi maadili ya kampuni yetu.”
Chanzo cha picha, EPA
Kampuni ya Hallmark inataka kurejeshewa pesa ilizotoa kwa wabunge wa Republican Seneta Josh Hawley (Missouri) na Roger Marshall (Kansas).
- Kampuni ya mtandaoni ya AirBnB ilishutumu vurugu hizo zilizotokea Washington DC, na kusema : “Tutapitia tena mpangokazi wetu upande wa hatua za kuchukuliwa na kusitisha ufadhili wetu kwa wale waliopiga kura ya kupinga kuidhinishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais.”
- Wengine ni kampuni ya bima ya Blue Cross Blue Shield, ambao mgao wao umewaendea wabunge wa Republican katika kila uchaguzi tangu mwaka 1996.
- Kampuni ya Boston Scientific ambao ni watengenezaji wa vifaa vya kimatibabu.
- Benki ya Commerce Bancshares.
Waliositisha ufadhili wao wote
Kampuni zingine zimechagua kusitisha ufadhili wa aina yoyote ile kwa waliopiga kura kuunga mkono matokeo pamoja na wale waliopinga kumuidhinisha Biden kama mshindi, hatua ambayo imeshangaza wengi na kuzua maswali kama kweli kuna demokrasia.
Kampuni hizo ni pamoja na kampuni kubwa za teknolojia za Facebook, Amazon, Microsoft na Google, pamoja na zingine maarufu kama Coca Cola, Verizon, benki za JPMorgan Chase, Citigroup na Goldman Sachs, mtungo wa hoteli ya Hilton, kampuni ya Charles Schwab inayotoa huduma za fedha na muungano wa makampuni ya 3M .
Chanzo cha picha, Reuters
Mtandao wa Facebook utachukua miaka mitatu ya kwanza 2021 kupitia tena sera yake ya ufadhili.
Kampuni zingine za utoaji wa kadi za manunuzi American Express na Mastercard pia nazo zimesema zinasitisha ufadhili wake bila kujali nani ataathirika na hatua hiyo.
Mbali na kampuni kidogo tu, nyingi hazijasema hatua yao waliochukua ya kusitisha ufadhili itatekelezwa hadi lini.
Hilo likiwa limetoa muda wa kutosha kwa makampuni hayo kuamua hatua za kuchukuliwa.