Kasuku wapatikana wamefichwa kwenye chupa za plastiki Indonesia


Kasuku hao walitolewa kwenye chupa hizo walipopatikana Fakfak katika jimbo la magharibi la Papua nchini Indonesia

Maelezo ya picha,

Kasuku hao walitolewa kwenye chupa hizo walipopatikana Fakfak katika jimbo la magharibi la Papua nchini Indonesia

Makumi ya kasuku waliokuwa wamefichwa kwenye chupa za plastiki na kusafirishwa kimagendo kwenye meli iliyokuwa ikienda nchini Indonesia wamepatikana meli hiyo ilipotia nanga katika mji wa bandari wa Fakfak magharibi mwa nchi hiyo.

Polisi wanasema wafanyakazi wa meli hiyo walipata kasuku 64 wakiwa hai na 10 wakiwa tayari wamekufa baada ya kusikia kelele kutoka kwenye sanduku moja kubwa.

Indonesia ni nyumbani kwa idadi kubwa ya spishi za ndege wanaokabiliwa na hatari ya kuangamia barani Asia kutoka na ongezeko la biashara haramu ya ndege hao.

Ndege wanauzwa katika soko la ndani ya nchi na kisha kusafirishwa kimagendo hadi ughaibuni.

Haijabainika mahali kasuku hao waliopatikana siku ya Alhamisi katika mji wa bandari wa Fakfak, msemaji wa polisi katilka eneo hilo Dodik Junaidi ameambia shirika la habari la AFP.

“Wafanyakazi wa meli hiyo wametuambia kuwa wanashuku kuna wanyama ndani ya sanduku hilo kutokana na sauti walizokuwa wakisikia kutoka humo ndani,” alisema siku ya Ijumaa.

Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kutokana na kisa hicho.

Hii sio mara ya kwanza ndege wamepatikana wakiwa wamefichwa ndani ya chupa za plastiki. Mwaka 2015 polisi nchi Indonesia walimkamata mtu aliyekuwa akijaribu kuwasafirisha kimagendo ndege 21 ambao wanakabiliwa na tisho la kuangamia ndani ya chupa za plastika.

Mwana 2017 mamlaka nchini Indonesia walipata ndege 125 waliokuwa wamefichwa ndani ya bombo la kupitisha maji baada ya kuendesha msako dhidi ya wanyamaporiSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *