Kenya: Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i azungumzia kuhusu mashambulizi ya kigaidi


Akizungumza katika kikao kikuu cha usalama mjini Mombasa waziri Matiang’i amesema vitengo mbali mbali vya usalama vilivyoko katika makao makuu ya usalama jijini Nairobi vitagawanywa katika makundi madogo amdogo kadhaa ambavyo maafisa wake watakuwa wakizuru kila kaunti angalau mara mbili kwa mwaka kujumuika na maafisa wa mashinani kufahamu na kupata suluhisho katika kukabili  changamoto mbali mbali zinazosababisha tishio la usalama nchini Kenya.

Matiang’i amesema  “Punde baada ya kikao hiki nitawaamrisha maafisa wakuu katika makao makuu ya usalama nchini kujigawanya katika makundi madogo mawili au matatu na wawe wakitembelea kila kaunti mara mbili kwa mwaka ama zaidi na kufanya kazi na maafisa wa usalama katika kaunti ili kujua ni shida gani wanazozipitia na nikupitia njia hiyo ndio tutaweza kujua kinachoendelea mashinani “.

Nchini Kenya kuna vitengo mbali mbali vya usalama lakini taifa hilo limekuwa likikabiliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Al Shabbaab na pia makundi ya wahuni katika sehemu mbali mbali za taifa hilo, ni kutokana na hilo waziri Matiang’I amesema wanataka vitengo hivyo kuwa pamoja katika kufanya kazi ikiwa ni kushirikiana katika kupeana taarifa za kijasusi, utumiaji wa vifaa sawa na kuweka malengo na mipango ya kila mwaka ya kukabiliana na ukosefu wa usalama.

Katika kikao hicho katibu mkuu wa wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho amesema kwamba kikosi cha pamoja cha idara za usalama kimetayarishwa kwa ajili ya kukabiliana na usalama wa ndani sawa na wahalifu wanaoingia kupitia mipakani.

Baadhi ya mataifa ya Ulaya yamewatahadharisha wananchi wake kutozuru kaunti ya Lamu ambayo imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na kundi la kigaidi la Al Shabbab ambalo lina maficho ya kambi zake ndani ya msitu mkubwa wa Boni ulioko katika kaunti ya Lamu.

Mwaka 2014 Al Shabbb waliua kiasi yaa watu sitini katika eneo la Mpeketoni, Lamu jambo lililolazimisha serikali kupeleka Jeshi la Kenya ndani ya msitu wa Boni kuwafurusha wanamgambo hao lakini hadi wa leo msitu huo bado ni makao ya Al Shabbab.

 

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *