Kenya yamtema Mfaransa Migne


Migne, mwenye umri wa miaka 46, amesifiwa kwa kazi nzuri na ustadi wa kiwango cha juu vilivyopelekea timu hiyo ya taifa ya Kenya kuingia katika kinyang’anyiro cha Kombe la Mataifa ya Afrika (CAF) mwaka huu nchini Misri.

Ilikuwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 15 kwa Harambee Stars kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

FKF inasema utaratibu wa kumteuwa atakayeshika nafasi ya Migne umeshaanza na kuelezea matumaini ya kumtangaza atakayeshika nafasi hiyo hivi karibuni.

Migne aliiongoza Harambee Stars kwa muda wa miezi 15 lakini enzi yake imemalizika kwa kupoteza mechi kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya Tanzania kuweza kuwakilishwa katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika mwaka 2020.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *