Kesi ya genge kubwa la uhalifu yaanza kusikilizwa Italia


Prosecutor Nicola Gratteri arrives at the High Security Courthouse

Maelezo ya picha,

Mwendesha mashtaka anayepinga magenge ya uhalifu Nicola Gratteri ameapa kuangamiza ‘genge la Ndrangheta”

Mamia ya raia wa Italia ambao ni wanachama wa genge la uhalifu lenye nguvu zaidi nchini humo watafikishwa mahakamani kwenye kesi ya uhalifu ambayo haijawahi kufanyika katika kipindi cha miongo kadhaa.

Wanachama wa genge hilo pamoja na maafisa wafisadi 355 walishtakiwa baada ya genge la uhalifu la ‘Ndrangheta’ kufuatiliwa kwa muda mrefu.

Zaidi ya mashuhuda 900 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao na baadhi ya makosa yanayowakabili ni pamoja na mauaji, ulanguzi wa dawa za kulevya, unyang’anyi na utakatishaji wa fedha.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa Jumatano na inatarajiwa kuchukua kipindi cha miaka miwili.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *