Kifaa kilichotengenezwa kwa ajili ya kufichua jinsia chalipuka na chamuua mwanaume


Picture of Christopher Pekny, taken from his Facebook page

Maelezo ya picha,

Kaka yake Christopher Pekny Peter ameiita ajali hiyo “kituko kikubwa”

Mwanaume mmoja kutoka New York amefariki baada ya kifaa alichokuwa akikitengeneza kwa ajili ya kutumiwa katika sherehe ya kutambulisha jinsia kulipuka , kwa mujibu wa polisi.

Christopher Pekny, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akitengeneza kifaa katika mji wa Liberty wakati kilipolipuka Jumapili mchana.

Polisi inasema mlipuko huo huo ulimuua Pekny na kumjeruhi kaka yake Michael Pekny, mwenye umri wa miaka 27, ambaye alipelekwa hospitalini.

Sherehe za kutangaza jinsia ni sherehe ambapo wazazi hutangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kike ama wa kiume.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *