Kombora la ajabu: Je ni silaha gani iliofanyiwa majaribio na Urusi Arctic?


Jaribio la kombora la Burevestnik- kutoka kanda ya video ya Urusi

Haki miliki ya picha
Russian defence ministry

Wahandisi watano wa nguvu za kinyuklia waliofariki kufuatia kulipuka kwa injini ya roketi wamezikwa mjini Sarov, yapata kilomita 373 mashariki mwa mj kuu wa Moscow ambapo vichwa vya nyuklia hutengezwa.

Shirika la serikali la usimamizi wa nguvu za kinyuklia nchini humo Rosatam lilisema kwamba wataalam hao walikuwa wakijaribu injini ya nyuklia.

Lakini halikutoa maelezo zaidi ya kiufundi.

Jaribio hilo lilifanywa karibu na ufukwe wa bahari ya Arctic. Urusi imekuwa ikijaribu kombora la kinyuklia kwa jina Burevesnik.

Lakini maafisa hawakuelezea ni mfumo gani uliotumika katika jaribio hilo la siku ya Alhamisi.

Mlipuko huo ulifuatiwa na kupanda kwa mionzi katika eneo la Seberodvinsk, mji uliopo yapata kilomita 40 mashariki mwa Nyonoksa karibu na bahari nyeupe.

Maafisa wa Severodvinsk wanasema kwamba mionzi hiyo ilifikia Microsierverts 2 kwa saa , kabla ya kurudi katika hali ya kawaida ya 0.11 Microsieverts.

Viwango vyote viwili ni vidogo mno kusababisha ugonjwa unaosababishwa na mionzi.

Wahandisi wengine watatu walijeruhiwa katika mlipuko huo na sasa wako hospitalini , Rosatom alisema.

Wataalam wa Urusi na magharibi wanasema kuwa jaribio hilo lilihusihswa na ndege wa baharini kwa jina Petrel.

Rais Vadmiri Putin alielezea kombora hilo katika hotuba yake bungeni mwezi Machi 2018.

Nato imelipatia umbo la SSC-X-9 Skyfall.

Mark Galeotti, mchanganuzi mkuu na mtafiti katika taasisi ya Rusi anasema kwamba urushaji wa kombora la kinyuklia unakabiliwa na changaomoto za kiufundi .

Kuna kasi dhidi ya uzito wa mfumo mbali na hatari ya kombora hilo kutoa mionzi kila mahali linapopitia , aliambia BBC.

Mfumo huo mpya ulianzishwa nyakati za Usoveiti – zilizotolewa zilikokuwa zikihifadhiwa na kuimarishwa . Injini ya Burevestnik inayoweza kurusha kombora la kinyuklia hauna uwezo wa kurusha kombora mbali kulingana na bwana Putin.

Lakini mlipuko wa Nyonoksa unaweza kuwa ulihusisha silaha nyengine ambayo pia ina uwezo wa kirusha kichwa cha nyuklia.

Ni nini kinachojulikana kuhusu mlipuko huo?

Wahandisi hao watano waliofariki walikuwa wataalam na mashujaa ambao walijua hatari zinazowakabili na walikuwa wamefanya majaribio mengine katika mazingira magumu zaidi alisema afisa mwanadamizi wa Rosatom Valentin Kostyukov .

Anaongoza kituo cha nyuklia cha Sarov – kituo kilichotumika wakati wa vita baridi kinachohusishwa na bomu lililotengezwa na hydrogen bomb nchini Urusi.

Aliwataja wahandisi hao kuwa Alexei Vyushin, Yevgeny Korotayev ,Vyacheslav Lipshev, Sergei Pichugin , Vladislav Yanovsky.

Awali wizara ya ulinzi ilikuwa imesema kwamba jaribio hilo lilihusisha injini yenye radio – isotope na lilifanyika katika ufukwe wa bahari.

Awali wizara hiyo ya ulinzi pia ilikuwa imesema kwamba mlipuko huo wa tarehe 8 Agosti ulihusisha injini ya roketi inayoendeshwa na maji na kutoa idadi ya waliofariki kuwa wawili bila ya kuelezea.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Jaribio la Nyonoksa lilianzishwa miaka ya Usovieti

Kabla ya kichwa hicho , wizara ya ulinzi ililitangaza eneo La Dvina Bay kuwa eneo ambalo watu hawahitajiki kuwepo na kwamba litasalia kufungwa hao hadi mapema Septemba.

Je kombora hilo linalotumia nguvu za kinyuklia ni ugunduzi mpya?

Mark Galeotti wa Rusi anasema kwamba kuna uvumi kwamba huenda injini hiyo ya Burevestnik lsifaulu.

Anasema kwamba kombora jingine la Urusi , la Bulava lilifeli mara kadhaa wakati wa majaribio yake.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Jumba la makumbusho la Sarov (1997 photo) lina mifano ya bomu la Gydrogen lililotumika na UrusiSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *