Kongamano la Nato: Boris Johnson kushinikiza umoja wa muungano huo unapoadhimisha miaka 70


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson. Picha ya: Decemba 2, 2019

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Boris Johnson atakuwa mwenyeji wa kongamano la viongozi wa dunia hlicha ya kampeini ya uchaguzi kuchacha nchini Uingerezacampaign

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ni mwenyeji wa viongozi wa muungano wa kujihami kwa mataifa ya magharibi, Nato wanaokutana mjini London kuadhimisha miaka 70 tangu muungano huo ulipobuniwa licha ya taharuki inayozidi kuongezeka.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Jumanne karibu na mji wa London unakuja wakati ambapo kuna mvutano kati ya Ufaransa na Uturuki na mjadala unaoendelea kuhusu ufadhili wa Nato.

Mwezi uliopita, rais wa Ufaransa aliitaja Nato kuwa muungano ”usio na maana”, akisema kuwa wanachama wake hawashirikiani kuhusu masuala muhimu.

Rais wa Marekani Donald Trump ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mkutano huo.

Aliwasili nchini Uingereza siku ya Jumatatu kabla ya hafla maalum itakayoandaliwa na malkia katika kasri la Buckingham Palace Jumanne jioni.

Bwana Trump pia anajiandaa kufanya mazungumzo ya pembeni na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na katibu mkuu wa Nato.

Hali ya taharuki imekuwa ikipanda tangu rais Trump, alipolalamika mara kadhaa kuwa mchango wa mataifa ya Ulaya ambayo ni wanachama wa Nato haukidhi mahitaji ya shirika hilo ambalo lilibuniwa kukabiliana na vitisho baada ya vita vikuu vya pili vya dunia ili kupanuka kwa ukomyunisti baada ya vita vya pili vya dunia.

Mkutano huo unafanyika wakati ambapo rais Trump anakabiliwa na uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi yake huku akijiandaa kwa kampeini ya uchaguzi mwaka ujao.

Huku hayo yakijiri Uingereza inaelekea kufanya uchaguzi mkuu wiki ijayo licha ya mchakato wa nchi hiyo kujiondoa kutoka muungano wa ulaya maarufu Brexit .

Wanachama wa Nato wameahidi kusaidiana endapo moja kati ya washirika wake 29 atashambuliwa.

Boris Johnson atasema nini?

Kama mwenyeji wa kongamano hilo la siku mbili, Bwana Johnson anatarajiwa kutilia mkazo umuhimu wa umoja wa Nato, kama “nguzo ya usalama katika kanda ya Euro-Atlantic “ambayo inasaidia” kuweka watu bilioni moja”, msemaji wake alisema.

“Msimamo wa waziri mkuu ni kwamba Nato ni muungano thabiti wa kijeshi ambao historia ya ufanisi wake unatokana na jinsi inavyoshughulikia hatari inayotukabili katika ulimwengu wa sasa,” msemaji wa waziri mkuu aliongeza.

“Waziri mkuu atawasisitizia wanachama wote kushirikiana katika masuala yaliyopewa kipaumbele ili Nato iweze kushughulikia mapema changamoto zozote zitakazoibuka.”

Kabla ya ziara yake, rais Trump aliandika katika Twitter kujipongeza kuhusu tamko la hivi karibuni la katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg la kuongeza bajeti.

Nato inakadiria kuwa kufikia mwaka 2019 ni mataifa manane miongoni mwao Marekani ndio yalioafikia viwango vya mchango uliowekwa kama ilivyokubaliwa na mataifa wanachama.

Mataifa hayo yalikubaliana kwamba yatumie 2% au zaidi ya pato la jumla la serikali kwa ulinzi.

Bwana Stoltenberg siku ya Ijumaa alisema kufikia 2020, washirika wa Ulaya na Canada watakuwa wamewekeza dola bilioni 130 sawa na (£100bn) zaidi tangu 2016, mwaka ambao rais Trump alichaguliwa.

Haki miliki ya picha
AFP/Getty Images

Image caption

Je Bwana Erdogan (kushoto) na Bwana Macron watajaribu kusuluhisha mzozo kati yao?

Masuala mengine ni yapi?

Katika mahojiano mwezi uliopita Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliuelezea Muungano wa Nato kama “ubongo” uliokufa, akisisitiza kile anachokiona kama kutokuwa na utashi wa mdhamini mkuu wa Marekani kwa Muungano huo wa kujihami wa nchi za magharibi.

Alitaja hatua ya Marekani kuondoa vikosi vyake kaskazini mwa Syria bila kushauriana na muungano huo mwezi Octoba, na kuipatia nafasi Uturuki kuvamia kijeshi maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa Kikurdi ili kubuni “eneo salama” katika mpaka wake.

Hatiua hiyo ya kijeshi ilizorotesha uhusiano kati ya Uturuki na wanachama wengine wa Nato.

Ijumaa iliyopita, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alijibu tamko la Macron akisema kuwa yeye ndiye “amekufa akili”. Alimkosoa akisema kuwa “ni mgonjwa na mwenye uelewa mdogo” kuhusiana na ugaidi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *