'Kuna siasa, uchumi na mchezo wa kimkakati nyuma ya chanjo za corona unaoweza kuleta maafa'


Richard Haass

Maelezo ya picha,

Kulingana na Richard Hass, tatizo la kukabiliana na ”chanjo ya utaifa” ni kwamba itawaacha mabilioni ya watu wakiwa katika hali ya hatarini

Mbio za kupata chanjo dhidi ya chanjo dhidi covid-19 zimeshika kasi , huuMataifa kadhaa yenye nguvu kama vile Marekani, China na Uingereza yanapimana nguvu za uwezo wao wa kisayansi kwa namna yoyote ile ili kupata chanjo itakayokabili virusi vya corona.

Kwasababu haiwezekani kubashiri ni chanjo gani itakayokuwa ya kwanza kufikia lengo la kwanza, nchi zilizoendelea sasa zimeanza kununua mamilioni ya dozi za chanjo zinazoweza kufanikiwa kutimiza vigezo vya chanjo kutoka kwa maabara tofauti kujaribu kuhakikisha wanaweza kusambaza chanjo hizo kwa watu wao.

Kwa mfano , Uingereza imesaini makubaliano na makampuni ya wasambazaji kadhaa wanaoweza kusambaza chanjo kama vile : AstraZeneca, Pfizer and BioNtech, na kampuni ya Valneva.

Hivyo hivyo. Marekani imefanya mikataba na makampuni kama vile Pfizer na BioNTech; Moderna ana Johnson & Johnson; AstraZeneca, na Novavax.

Suluhu hizi za kibinafsi, ambazo sio sehemu ya mapatano baina ya nchi, yanaweza kuelezewa kama “chanjo ya utaifa”.

Katika mahojiano na BBC, Richard N. Haass , Rais wa baraza la mahusiano ya kimataifa (CFR), na Mkurugenzi wa sera ya mipango katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani , mjumbe maalum wa Ireland ya Kaskazini na mratibu wa mpango wa “Afghanstan ijyato “, anafafanua zaidi juu kile alichomaanisha alipoandika kuwa: ”Kuna kisiasa, uchumi na mchezo wa kimkakati nyuma ya chanjo za corona vinavyoweza kuleta maafa ”

Alisema: ”Tunashuhudia utaifa wa chanjo ya covid-19 ambao unaweza kuelezewa kama kinga ya utaifa”

Serikali zimejitayarisha binafsi na sababu iko wazi. Mataifa yanakabiliwa na shinikizo ya kutoa dozi za chanjo kwa raia wao.

Maelezo ya picha,

Mataifa yenye nguvu zaidi duniani yamesaini mikataba ya mamilioni ya dola na maabara ili kuhakikisha yanakuwa na chanjo za kutosha dhidi ya virusi vya corona

Lakini anasema tatizo ni kwamba mipango ya nchi zenye nguvu itawaacha mabilioni ya watu katika hali ya kutokuwa na uwezo wa kupata chanjo, jambo ambalo ni mzozo.

Lakini pia itakua na athari mbaya kwa serikali ambazo zitatumia chanjo za utaifa kwasababu kama kuna idadi kubwa ya watu walioambukizwa corona duniani, ikizingatiwa kwamba kuna utandawazi, ugonjwa utaendelea kusambaa.

Kwahiyo, kuna siasa, uchumi na mchezo wa kimkakati nyuma ya chanjo ambao matokeo yake ni mkasa.

”Ninaweza kuuita ushindani kwa ajili ya chanjo, sio vita. Kila mmoja anataka kupata chanjo kwanza. Baadhi kwasbabu za kisiasa, lakini wengi kwasababu za kisiasa zaidi” , anasema Richard N. Haass.

Maelezo ya picha,

“Viongozi wanakabiliwa na shinikizo la kutoadozi za chanjo kwa raia wa nchi zao wenyewe,” Haass anasema , hii inazifanya nchi kuona ugumu kusaini mikataba shirikishi na mataifa mengine

”Tatizo ni kwamba soto tumo katika hali ya hatari iwapo kutakuwa na watu wengi wenye maambukizi . Hilo ni funzo kubwa tulilolipata kutokana na ugonjwa huu.” Anasema Richard N. Haass,

Hata kama nchi moja tu iko mbele ya nchi nyingine katika kutengeneza chanjo, bado watalazimika kutegemea nchi nyingine, kwasababu huenda wakahitaji kuagiza baadhi ya bidhaa ili waweze kutengeneza chanjo.

Sidhani kama kuna nchi yoyote ambayo inajitosheleza kwa asilimia 100 katika kutengeneza chanjo kwasababu watahitaji aina fulani ya kemikali au kiungo fulani cha chanjo kutoka nchi nyingine, anasema.

Je ni lipi linaweza kuwa suluhu la tatizo hili ?

Sababu kuu ya kufikiria tofauti juu ya jambo hili ni hii.

Richard N. Haass anasema yanapaswa kuwepo makubaliano ya dunia, ambapo serikali inakubali juu ya njia za kushirikisha nchi nyingine chanjo . Kwa mfano kila serikali ikubali kuchukua nusu ya chanjo na kutoa nusu nyingine kwa mataifa mengine duniani.

Maelezo ya picha,

“Tunashuhudia utaifa wa chanjo dhidi ya covid-19 anasema Richard Haass

Habari njema ni kwamba kama kuna makubaliano ya aina hiyo , na nchi haikua ya kwanza kutengeneza chanjo , utaweza kupata sehemu ya chanjo hiyo.

Je hilo linaweza kufanyika ?

Hapana. Huenda lisifanyike. Nchi kama vile Marekani , China na huenda wengine wanaamini kwamba wana fursa nzuri ya kutengeneza chanzo wakiwa ni wa kwanza lakini wanachokiwaza ni kutoa chanjo kwa watu wao.

Wakati huu utaifa unaongezeka mno. Serikali zinawasiwasi kwamba kama zijtafikia makubaliani ya kushirikisha nchi nyingine chanjo zao, nchi zao zitakua katika hatari ya kubaki nyuma kisiasa.

Na pia wazo la kuwa nchi ya kwanza kutengeneza chanjo ni mojawapo ya dalili kubwa zinazoonyesha kuwa nchi ina nguvu za kisiasa …

Taifa lolote litakalotengeneza chanjo likiwa la kwanza bila shaka litapata faida. Lakini huenda kile kitakachotokea ni kwamba kutakua na chanjo kadhaa na hakuna chanjo yoyote kati ya hizo itakua suluhu ya corona.

Chanjo zote zitakua na ukomo , wa idadi ya watu wanaoweza kusaidiwa, pamoja na athari zake.

Kinachoshangaza juu ya mjadala huu ni kwamba watu wanafikiri kuwa pale chanjo itakapopatikana itakua ni sawa na kupata medali ya dhahabu , kwamba itakua ni kama zawadi kubwa itakayotatuza tatizo la covid-19.

Na jibu ni hapana. Historia ya chanjo inaonesha kuwa chanjo inapopatikana, huwasaidia watu fulani , lakini si wote. Kwa hiyo itawasaidia watu kwa muda wa kipindi fulani. Itasababisha athari zisizotakikana na wengi watakataa kuchanjwa.

Maelezo ya picha,

“Kama hatutakua na busara ya kuwashirikisha watu wengine duniani chanjo , virusi vitaendelea kuwepo ,” anasema mtafiti .

Richard N. Haass anasema ”Utabiri wangu ni kwamba hata kama chanjo moja au zaidi zitapatikana bado tutahitajika kuendelea na agizo la watu kutokaribiana(social distancince, Kuvaa barakoa na kunawa mikono yetu na kuchukua tahadhari nyingine . Watu wataongeza chumvi juu ya madhara ambayo chanjo zitakua nayo. Chanjo haitatunusuru dhidi ya virusi vya corona”

Je kutakua na hatari gani kubwa iwapo hapatakua na makububailiano baina ya nchi juu ya chanjo ?

Hatari kubwa ni hatari ya kijbinadamu anasema Richard N. Haass . Nchi nyingi huenda zikashindwa kutekeleza madai ya kiafya na kiuchumi . Na kama hatutashirikishana chanjo kwa busara, virusi vitaendelea kuathiri idadi kubwa ya watu , na hiyo ina maanisha kwamba sote tutakua hatarini.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *