Kuna tija kwa vyama vya upinzani kususia uchaguzi?


Zitto Kabwe

Image caption

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuomba ushauri kwa umma kuwa wachukue hatua gani?

Zitto amesema kuwa kwa upande wao ACT-Wazalendo, jumla ya wagombea wote walikuwa 173,593 kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Mitaa 2,481, vijiji 8,218, Vitongoji 35,457 na wagombea wa nafasi za ujumbe wa halmashauri za vijiji na kamati za mtaa walikuwa 135,675.

Lakini wamebakiza asilimia nne ya wagombea wote walioweka na wagombea 166,649 wameondolewa.

Zitto Kabwe ametoa kauli hiyo mara baada ya chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema kutangaza kuwa kimejitoa katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaondelea nchini humo.

Mwenyekiti wa chama hiko cha upinzani alitangaza kutoshiriki katika uchaguzi unaotarajiwa kufanywa baadae mwezi huu kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuendeleza uonevu unaofanywa katika mchakato wa uchaguzi huo.

”Katika misingi hii ndugu watanzania, tumelazimika kukaa na kutafakari, baada ya vikao tulivyofanya kwa siku nzima ya leo, tumeamua kutobariki uchaguzi huu, ubatili umefanywa na serikali, na chama cha mapinduzi, sisi kama chama hatutashiriki katika uchaguzi huu, hatuko tayari kujihusisha na ubatili”, anasema Mbowe mwenyekiti wa chadema mara baada ya mkutano wao wa kamati kuu.

Hatua hii imeibua mjadala wenye sura mbili ambapo wengine wanaona kuwa sio jambo jema kwa upinzani kuchukua uamuzi huo na wengine kuhoji kama ni makubaliano ya wagombea wote.

“Mkisusa wenzenu wanakula !! Mnatengeneza njia ngumu sana kurudi bungeni 2020 !! Serikali za mitaa hamtakuwa na muwakilishi hata mmoja nchi nzima !! Nani atawaongoza au kusikiliza kero za wakereketwa wa CDM. Uvumilivu ni somo zuri !!” aliandika mshiriki mwingine.

Aidha serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi imesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ulivyopangwa tarehe 24 mwezi Novemba mwaka huu.

Ufafanuzi huo umetolewa mapema hii leo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni, Dodoma ambapo Mbunge wa Singida Kaskazini Justice Monko alitaka ufafanuzi wa serikali hasa baada ya Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema kutangaza kujitoa rasmi katika mchakato wa Uchaguzi huo.

“Tumesiki chama kikuu cha upinzani Chadema kimejitoa katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mtaa, hivyo kuwakosesha wananch haki zao za kimsingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Je serikali ina kauli gani kutokana na kadhia hii?” aliuliza Justice Monko ambae ni mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini.

Akijibu swali hilo, naibu waziri wa Tamisemi Mwita Waitara Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Tamisemi mapema hii leo, amevitaka vyama vyengine kuendelea na mchakato wa kushiriki katika uchaguzi.

“Tulieleza na kurudia mara kadhaa kwamba watu wenye sifa ya kutuma mapingamizi ni wale ambao ni wagombea, wenzetu walitaka watoe kauli bungeni, kwenye mitandao, mtaani na serikali iamue. Serikali inafanya kazi kwa mawasiliano, hatuna document mezani, hatuwezi kujadili jambo, lakini nitoe wito, yale maagizo ya kutoa kwamba wanahamasisha wananchi wasishiriki katika shughuli za maendeleo, mwenye mamlaka ya kutoa maelezo nchini ni rais pekee na sio kiongozi wa chama cha siasa, kiongozi wa chama anatoa maagizo kwa wanachama wake,” alisema naibu waziri Waitara.

Wakati huo huo, ametoa wito kwa wakuu wa wilaya kumchukulia hatua yeyote ambae atabainika kuhamasisha vurugu.

“Nitoe maelekezo kwa wakuu wa wilaya ambao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama, tumepata taarifa kwenye mitandao, wanahamasisha watu wanaharibu mazao ya watu, wanatishia watumishi wa umma, wakuu wa wilaya popote mlipo kama kuna mtu anahisi hakutendewa haki katika uchaguzi huu na anafanya fujo, sheria stahiki zichukulie mkondo wake.”

Image caption

Freeman Mbowe kiongozi wa chama cha upinzani Chadema

Haya yanajiri baada ya mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutangaza kujitoa rasmi katika mchakato huo kwa madai kwamba, demokrasia ‘imebakwa’.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma hapo jana, Mbowe alisema, “Chama kinaendelea kutafakari kichukue hatua gani za kufuata lakini maelezo mahususi ambayo tunawaeleza wanachama wetu hatushiriki chaguzi hizi, wote wajitoe na wasitambue viongozi wote watakaopatikana katika serikali za vijiji, vitongoji na serikali za mitaa, na hiyo ni hatua ya kwanza tusilaumiane.”

Baada ya zoezi hili la uchukuaji na urudishaji fomu kukamilika, hatua inayofuata ni ile ya kuanza kampeni kwa wagombea mbalimbali ambapo zitaendelea kwa muda wa wiki moja.

Hatua hii ya Chadema kususia uchaguzi imepokelewa kwa hisia tofauti huku baadhi wakihoji iwapo hatua hiyo itakuwa na tija yoyote.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *