Kuondolewa marufuku kwa wasichana wa shule wanaopata mimba kwaibua hisia mseto Tanzania


v

Hatua ya Serikali ya Tanzania kuondoa marufuku ya wanafunzi wanaopata ujauzito kurejea masomoni, imepokelewa kwa mtazamo tofauti kwa wale waliokuwa wanaonekana kuunga mkoano na wale waliokuwa wanapinga. Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika miaka 60 ya uhuru wa Taifa hilo.

Mbali na wanafunzi waliopata mimba, wanafunzi wengine waliokatiza masomo ya kwa sababu mbalimbali nao wataruhusiwa kurejea katika mfumo huo rasmi.

Rebecca Gyumi, Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wasichana Tanzania, Msichana Initiative, ameiambia BBC kwamba hatua hiyo ya serikali wameipokea vizuri ila bado kuna wasiwasi kidogo

‘tumepokea kwa furaha sana , na niseme tu tunatumaini waraka ambao mheshimiwa waziri amehaidi atautoa, utakaoelezea utekelezaji wa tamko lake, itaweza kutupa picha ya namna ambayo serikali imejipanga kutekeleza hili’, alisema Gyumi na kuongeza kuwa inapaswa kuwekewa sheria hili tamko la waziri na waraka wake uwe na nguvu za kisheria.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *