Kurasa zaTwitter zilitapakaa video ya mwanaume akimvisha mpenziwe pete kwenye mgahawa wa KFC


Chakula cha KFC

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Hashtag #KFCProposal ilianza kusambaa mitandaoni dunia nzima

Raia wa Afrika Kusini wametoa ofa kuwasaidia wenza kufanya sherehe ya ndoa waliokuwa wakiItamani siku zote baada ya picha ya video za mwanaume aliyekuwa akimuomba mpenzi wake kwenye mgahawa wa chakula KFC wafunge ndoa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Video hiyo ilimuonesha mwanaume akiwa amepiga goti na kutoa pete kwa mpenziwe wakati walipokuwa wakila kuku.

Mgahawa wa KFC ulisambaza video hiyo ikiomba msaada wa kuwatafuta wenza hao.

Posti ya KFC kwenye mtandao wa Twitter ilitawanywa zaidi ya mara 17,000 kwa hashtag #KFCProposal ilianza kuwa maarufu mitandaoni.

Baadae wenza hao walifahamika kwa majina Bhut’ Hector na Nonhlanhla. lakini haikuishia hapo tu.

Baada ya muda mfupi watu waliokuwa hawafahamiani na wapenzi hao walianza kutoa ahadi ya kuwasaidia kupanga siku yao ya harusi, ikiwemo malazi wakati wa fungate na kutumbuiza siku ya sherehe.

”Ningependa kutoa ofa ya kutumbuiza kwenye harusi bure…Ninapenda mapenzi” aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, msanii maarufu na mtunzi Zakes Bantwini.

Huwezi kusikiliza tena

Athari za mitandao ya kijamii katika maandalizi ya harusi

Kisha makampuni yakaanza kutoa zawadi.

”Maeneo ya fungate yanaonekana kuwa mbali. Mtu atahitaji kuwapeleka huko.Tutashughulikia,” akaunti ya twitter ya kampuni ya magari ya Audi ya Afrika Kusini ilieleza

”Tungependa muungano wao uwe wa kipekee kwa kuwapa kurasa mbili za kwenye jarida letu ili waeleze hadithi yao nzuri ya mapenzi! jarida la DRUM liliandika kwenye ukurasa wa Twitter.

Ofa za kila kitu kuanzia vilevi mpaka masufuria ya kupikia nguo za michezo zilijitokeza siku ya Ijumaa, sambamba na michango ya maelfu ya pauni.

Kateka Malobola, mpita njia ambaye alirekodi picha ya video na kuiweka kwenye mtandao wa kijamii, alizungumzia furaha yake isiyo kifani kutokana na mchango wa raia wa nchi hiyo.

” Nilirekodi video hiyo na kuipeleka kwenye kikundi cha WhatsApp nikisema ‘tazameni’! kisha nikaiweka kwenye mtandao wa Facebook na Instagram, na kisha Boom! ” alieleza.

Wapenzi hao wamewashukuru wote wanaowatakia heri walipozungumza na kipindi cha Sowetan LIVE.E.

Wapenzi hao pia wameiambia tovuti kuwa awali walioana mwaka 2012, lakini bwana harusi hakuridhika na pete alizonunua wakati huo na kutaka kumnunulia mke wake kitu kizuri zaidi.

”Sifanyi kazi hivyo sikuwa na fedha za kutosha kumpa Nonhlanhla harusi nzuri, mapambo ya vito lakini nilitaka kufanya kitu kidogo,”Hector alisema.

”Asante Afrika kusini. Ukarimu wenu umetugusa kwa kweli. Hatukufikiria kuwa hadithi yetu ya mapenzi ingewagusa wengi weny,” waliongeza wapenzi hao.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *