Kwanini Kardashian alijaribu kufuta picha yake mtandaoni?


Khloe Kardashian

Chanzo cha picha, Getty Images

Anatoka katika moja ya familia maarufu zaidi katika ulimwengu wa burudani na ni mara chache Khloe Kardashian amewahi kupigwa picha akiwa na muonekano ambao thamani yake kipesa ni chini ya mamilioni ya dola, yaani muonekano wa kawaida tu.

Nyota huyo wa televisheni na mwenye ushawishi katika mitandao ya kijamii na timu yake kwa kawaida huwa na utaalamu wa kuonesha picha nzuri hasa walizopigwa kwenye umma.

Na hivyo basi baada ya picha yake ya kawaida tu kusambazwa kwenye mtandao wake wa kijamii ” kwa bahati mbaya” walifanya kila wanaloweza kuiondoa mtandaoni.

Wametaka majukwaa ya mitandao ya kijamii kuindoa picha hiyo, ingawa juhudi hizo zimechochea wengine kuisambaza hata zaidi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *