Kwanini kina mama walanazimika kuuza watoto wao Venezuela


A sign reading "Dumping babies is forbidden "

Haki miliki ya picha
Guillermo D. Olmo

Image caption

Ishara hii ni ya kuvutia nadhari juu ya idadi ya watoto wanaoendelea kutelekezwa

“Kutupa watoto ni jambo lisilokubalika,” ishara hii iliyoundwa na Eric Mejicano inasema hivyo.

Msanii wa Venezuela alichora ishara hii na kuandika ujumbe huo kwenye kuta za majumba nchini Venezuela baada ya mtoto mchanga kupatikana ametupwa kwenye jaa la taka karibu na nyumba anayoishi mji wa Caracas.

Mejicano anasema kwamba alianzisha kampeni ya kutahadharsha watu kwamba Venezuela “hili jambo linaendelea kuchukuliwa kuwa la kawaida na haifai”.

Uchumi wa nchi hiyo unaporomoka na raia mmoja kati ya watatu wa Venezuela wanakuwa na wakati mgumu kupata chakula cha kila siku kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa.

Huku ikiwa vigumu kugharamia njia za kupanga uzazi na kufikia mahitaji mengi ya kifedha, mimba za mapema zimekuwa jambo la kawaida.

Sheria kali za uavyaji mimba ambazo zinaruhusu utoaji wa mimba iwapo tu maisha ya mama yako hatarini ama ikiwa kiumbe kilicho tumboni kinahatarisha maisha ya mama.

Huku mgogoro wa kiuchumi ukiendelea, shirika moja la utoaji msaada mwaka 2018, lilisema kwamba idadi ya watoto wanaotupwa na mama zao mitaani au wanaoachwa katika milango ya majengo ya umma ikiongezeka kwa asilimia 70.

Serikali ya Venezuela haijatoa idadi rasmi katika miaka ya hivi karibuni na wizara ya mawasiliano au shirika la serikali linalosimamia haki za watoto hakuna aliyejibu maombi ya kutaka kufanya mahojiano na BBC.

Lakini idara ya utoaji huduma ya jamii na wafanyakazi wa afya walizungumza na BBC na kuthibitisha kwamba kumekuwa na ongezeko la idadi ya watoto wanaotupwa pamoja na wale wanaotolewa kwa ajili ya kuasiliwa kwa njia isiyo rasmi.

Njia za Mkato

Nelson Villasmill ni mwanachama wa baraza la kulinda watoto katika maeneo masikini ya mji wa Caracas. Alielezea kwamba mfumo mbaya wa uasili unalazimisha wazazi walio na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo kutumia njia za mkato.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Maeneo ya watoto wasiojiweza kupikiwa chakula yameanzishwa lakini bado utapia mlo ni tatizo kubwa

Simulizi ya mtoto Tomás (ambaye sio jina lake kamili) ni moja ya visa hivyo. Alizaliwa na mama ambaye alikuwa maskini mjini Caracas ambaye alihisi hana uwezo wa kumlea.

Daktari wa wanawake aliyekuwepo wakati Tomás anazaliwa alikubali kusaidia.

Anasema hii haikuwa mara ya kwanza anakutana na mama ambaye anahisi hayuko tayari kulea mtoto. “Mara nyingi hubadilisha fikra zao mara ya kwanza wanaponyonyesha mtoto,” anaelezea. “Lakini mara nyingi hali huwa tofauti na hapo ndipo unapohitajika kutafuta suluhu.”

Aliwasiliana na mmoja wa wagonjwa wake ambaye ana umri wa miaka ya 40 na ana ndoto ya kuwa na mtoto, Tania ( ambaye sio jina lake kamili) hajafanikiwa kupata ujauzito.

Alitaka kumsaidia Tomás na mama yake lakini baada ya kufiria tena akaamua kuwasiliana na wanadoa ambao ni rafiki zae ambao walikubali mkumlea Tomás kama mtoo wake katika nyumba yao ya kijijini iliyopo Venezuela.

Mtoto huyo alisajiliwa haraka mno ili kuepusha maswali mengi kutoka kwa waja kwahiyo Tania akalipa rushwa ya $250 kwa afisa mmoja ili kumsajili rafiki yake kama mama mzazi wa Tomás.

Tomas kwa sasa analelewa na rafiki zake kijijini na familia yake mpya imesherehekea maisha mapya ya Tomás.

Tania amesema kwamba hajutii alichokifanya na kusisitiza kwamba aliamua kwenda kinyume na taratibu rasmi za kuasili mtoto kwa faida ya Tomás. “Sikuwa kufikiria kwamba nitaweza kufanya kitu kama hiki lakini sheria rasmi za kuasili mtoto Venezuela siyo rafiki na kitambo apate usaidizi, mtoto huwa ameteseka sana katika makao ya yatima,” anaelezea.

Kunaswa na kundi la usafirishaji haramu wa binadamu

Tomás alitolewa kwa familia nyengine baada ya mama yake kutoa idhini lakini kuwa watu wanaotumia vibaya hali ya kina mama kama hawa wa Venezuela walio katika uhitaji wa huduma ya aina hii.

Alipokuwa mjamzito na mtoto wake wa pili, mume wa Isabel aliaga dunia, na kumfanya Isabel ambaye sio jina lake halisi, afikirie kumtoa mtoto huyo kwa makao ya kulea yatima. “Nilikuwa peke yangu na nikaanza kuingiwa na hofu kwamba huenda nikashindwa kumlea mtoto wangu,” anasema.

Akaamua kufuatia ushauri wa mtu aliyekuwa anamfahamu, kwenda kisiwa cha Trinidad kukutana na wanandoa ambao aliarifiwa wanataka kumuasili mtoto wake.

Aliambiwa kwamba yeye ndiye atakayekuwa na uamuzi wa mwisho lakini baada ya kufika huko ghafla mambo yakabadilika na kupata shinikizo kutoka kwa mwanamke wa Colombia ambaye alikuwa anafanya maandalizi hayo.

“Niliarifiwa kwamba kila kitu kitafanyika chini ya sheria lakini sikuwa nimedhamiria kumtoa mtoto wangu,” anakumbuka. Lakini baada ya kufika Trinidad, “Nikagundua kwamba nimenaswa kwenye mtego wa usafirishaji haramu wa binadamu”.

“Kila wakati nilikuwa ninafuatiliwa,” Isabel anasema kwamba hakuruhusiwa kuondoka kwenye nyumba ambayo alikuwa anaishi na kwamba tikiti ya ndege ya kurejea ambayo aliahidiwa itamrejesha Venezuela wala hakuwahi kukatiwa.

Kutenganishwa na mwanawe

Isabel Wiki chache baadae akajifungua kabla ya wakati katika hospitali moja mjini Trinidad. Isabel akaamua kumtunza mtoto wake lakini yule mwanamke wa Colombia- kiunganishi kati yake na familia inayotaka kuasili mtoto na mwanamume mwengine ambaye alidai kuwa ni wakili wakaanza kumshinikiza.

“Waliniambia kwamba wazazi wake wapya walikuwa wanamsubiri kwenye sehemu ya kuegesha magari na kwamba sikuwa na budi zaidi ya kusaini nyaraka kadhaa kwa Kiingereza lugha ambayo sikuwa ninaielewa na kumpeana mtoto wangu.”

Mara ya kwanza Isabela alikataa lakini baada ya wiki kadhaa watu waliomshika waliongeza shinikizo na kuchukua chakula chake, dawa na nepi za kumbadilisha mtoto.

“Mwishoni, nililazimika kumtoa mtoto wangu ili kunusuru maisha yake na yangu na nikarejea Venezuela kutafuta usaidizi,” anasema hivyo akiwa analia.

Kwa usaidizi wa shirika moja lisilo la kiserikali, Isabel amefungua keshi ili kumchukua tena mtoto wake ambaye kwa sasa yuko chini ya mamlaka ya Trinidad.

Kwa sasa, anaruhusiwa tu kumuona kijana wake mara moja kwa wiki.

Anasema kwamba hatakata tamaa hadi atakapoungana tena na kijana wake.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *