Lazarus Chakwera: Rais wa Malawi 'aliyebishana na Mungu'


Lazarus Chakwera addressing a campaign rally (file pic)

Maelezo ya picha,

Bahati ya kisiasa ya Lazarus Chakwera ilimuangukia baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana

Katika mahubiri ya kipekee ya mhubiri ambaye ni rais mpya wa Malawi bwana Lazarus Chakwera, ametoa wito wa taifa kuwa na umoja mara to baada ya kuapishwa siku ya Jumapili.

Siku moja ya wiki ina inaonekana kumtosha kiongozi wa zamani wa kanisa la ‘Malawi Assemblies of God’, moja ya kanisa kubwa la kikristo nchini humo, ambalo amekuwa akihudumia kwa kutoa mahubiri ambayo wengi walivutiwa kwa maneno yake.

Taifa lilikuwa limegawanyika baada ya mgogoro uliotokea kwa kipindi cha miezi 13 kufuatia matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2019 kutiliwa shaka, na hivyo kupelekea mahakama kufuta matokeo.

Ukizungumzia utashi na mtindo ambao kiongozi wa kutetea haki za raia nchini Marekani , Martin Luther King, Rais Chakwera alizungumzia kuhusu ndoto ambazo zinawaunganisha pamoja na kufurahia utajiri na sio uhuru peke yake”.

Lakini alisema tena hakuna haja ya kuwa na ndoto.

“Wakati umefika kwenda mbali zaidi ya ndoto.

“Lazima wote tuamke kwa sababu huu ni wakati wa kuamka kutoka kwenye usingizi na kutimiza ndoto zetu kuwa kweli.”

Bwna Chakwera ni mwanaume anayemtumikia Mungu katika nchi ambayo ni ya kidini.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 65-alianza kupata uongozi kwenye chama cha Malawi Congress Party mwaka 2013 bila yeye kuwa na uzoefu wowote wa masuala ya kisiasa.

Kupambana na Mungu

Amepata mamlaka haya baada ya kuongoza kanisa la Mungu kwa miaka 24 lakini anakiri kuwa, aliwania nafasi ya urais kwa mara ya kwanza mwaka 2014, na jaribio hilo lilimpa maamuzi kuona kwamba kuwa mwanasiasa sio kazi rahisi.

“Ilinibidi kumuhoji Mungu anipe muongozo wa maisha ambayo hayakuonekana kuwa asili yangu, alisema hayo kwenye video ambayo ilichapishwa na kanisa la St Andrew’s Presbyterian huko California.

Lakini badala ya majadiliano mengi “Mungu alisema kuwa anatarajia kuwa ninaweza kuwamchungaji wa taifa zima'”.

Katika mahojiano mengine mwaka 2017, alisema katika mazungumzo yake na Mungu, alifungua biblia na kusoma sura ya tatu ya kitabu cha Kutoka, ambapo Mungu alimtokea Musa na kumwambia inabidi awaongoze Waisraeli watoke Misri.

Maelezo ya picha,

Matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2019, ambayo baadae yalifutwa, yalipingwa kwa maandamano

Hii inamuonyesha kuwa kiongozi anaweza kuongoza watu kiroho na katika mahitaji ya kijamii, mshauri wake Sean Kampondeni aliiambia BBC.

Lakini si kwamba anataka kubadili taifa la Malawi katika imani, aliongeza.

“Rais anaamini kuwa serikali ni kitu ambacho Mungu amekiweka katika mataifa ili kuhakikisha kuwa kuna utaratibu unafuatwa katika jamii ili binadamu wafanikiwe,” Bwana Kampondeni alifafanua.

“Nchini Malawi, anahisi kama taasisi ya serikali ilikuwa imeharibiwa kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita na kushindwa kutoa huduma na yeye yupo ili kuhakikisha kuwa kila mtu anaweza kujihudumia vizuri.”

Akihutubia taifa siku ya Jumapili, Bwana Chakwera ametokea mbali akiwa kijana aliyekulia kijijini ambako ni nje ya mji mkuu wa Lilongwe, ambao ulikuwa unagawanyika kwa aibu.

Mtoto wa mchungaji na mchungaji ambaye alianzisha makanisa kadhaa, alikuwa ametolewa nje ya ramani kabisa.

Lakini shule ya sekondari ya prestigious ambako alijifunza kutoka lafudhi yake kutoka kwa mwalimu raia wa Marekani,alikuwa anataka kuwa daktari .

Lakini alifikiria kama atakuwa daktari, hatakuwa na uwezo wa kuongea na watu wengi, alimwambia mwandishi wa habari Joab Chakhaza katika mahojiano ya mwaka 2017.

Unaweza pia kusoma:

Uongozi wa kisiasa na kiroho

Lakini wakati wa elimu yake , alisema alikutana na Mungu na akaanza kuongoza maisha yake ya uchungaji”.

Baba huyo wa watoto wane, anataka sasa kuwa na nguvu na maono na kuiongoza nchi.

Kwa wale ambao wanahisi kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya malengo ya uongozi wa kiroho na kisiasa hakuna bali nitofauti kidogo tu ,mshauri wa bwana Chakwera alisema rais anafahamu tosha jinsi ya kuwa mwanasiasa.

“Mtu yeyote anayeelewa michakato ya kisiasa na safari ya urais – siasa inakuwa haianzi wakati unaingia madarakani ,” Bwana Kampondeni aliiambia BBC.

“Lazima ufanye siasa nyingi kabla hujaingia katika ofisi za umma.”

Lakini alisema,uongozi wa rais huyu utakuwa tofauti, hatatumia mbinu chafu katika madaraka yake.

Inabidi atumie ujuzi wake ili kuunganisha watu wawe na umoja.

Maelezo ya picha,

Mshauri wa rais mpya alisema kuwa kuchaguliwa kulimfundisha Bwana Chakwera kuhusu jinsi ya kuwa mwanasiasa

Akihutubia taifa na sio tu wafuasi wake mjini Lilongwe, bwana Chakwera alisema wale ambao hawakumpigia kura wanaweza kuona urais wake kwa hofu na majonzi.

Lakini alijaribu kuwahakikishia kuwa wote ni wamoja.

“Malawi mpya ni nyumbani kwetu sote wakati wote nnapoiongoza nikiwa rais, hapa ni nyumbani ambako pia utajivunia.”

Mpinzani wa rais bwana Peter Mutharika, alishindwa kwa kura 59%, hivyo kuna wengi ambao wanaweza kuonekana kutomwamini, mwandishi Chakhaza aliiambia BBC.

kurithishwa ukabila

“Lakini vilevile ana kazi kubwa ya kukabiliana na ukabila ambao uko wazi katika kuchaguliwa kwake, kuna watu ambao wanahisi kama walitengwa haswa wake wa ukanda wa kati na mikoa ya magharibi ,” aliongeza.

Msukumo wa kujaribu kuweka usawa wa yaliyopita na watu yatakuwa yanaangaliwa kwa karibu kama kutakuwa na mabadiliko yoyote”.

Wafuasi wa rais wanaamini kuwa anaweza na atawapa wananchi wa Malawi utawala wa aina mpya ambao una msukumo wa Mungu na kuangazia mahitaji ya raia wake.

Katika kipindi hiki kigumu haswa, maamuzi magumu yatahitajika kuhakikisha mambo yanaenda, ukiachia uhusiano wa changamoto ya virusi vya corona, lakini pia kuna suala la kukabiliana na rushwa na kukuza kwa uchumi.

Changamoto zote hizo zitakuwa jaribio tosha kupima uwezo wake.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *