Maalim Seif agusia mwongozo wa ACT-Wazalendo


Akitoa maelekezo hayo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Vuga Mjini Unguja, Mshauri Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema wamelazimika kutoa muongozo huo, kutokana na vitendo vinavyofanywa na watu wanaokusudia kuharibu majengo na kushusha bendera za chama hicho katika matawi ya Unguja na Pemba.

Katika hatua nyengine Maalim Seif ameliomba jeshi la polisi kutenda haki katika utendaji wa kazi zake bila ya upendeleo, kwa kuwa linapaswa kuwahudumia wananchi wote bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Akionesha utulivu wa kuongea, Maalim aligusia miaka mitano ya utulivu na amani uliokuwepo chini ya Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ulioasisiwa na yeye mwenyewe pamoja na aliyekuwa Rais wa Zanzibar Amani Karume ambapo alisema waliingia kwenye maridhiano kwa kujali zaidi maslahi ya Zanzibar na wazanzibari kwa ujumla.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *