Maandamano Kinshasa: Raia walalamikia ukosefu usalama mashariki mwa DR Congo


maandamano DRC

Haki miliki ya picha
BBC/Mbelechi Msochi

Maandamano makubwa yamefanyika mjini kinshasa mbele ya ofisini ya rais wa Etienne Tshisekedi kumshinkiza atimize ahadi yake ya kampeni ya kuimairisha usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Haya ni kufuatia kuuawa kwa watu saba leo Jumatatu katika eneo hilo la mashariki linalotazamwa kama ngome ya uasi.

Zaidi ya raia mia moja kutoka eneo hilo la mashiriki ya Congo waliandama mbele ya ofisi ya rais Felix Tshisekedi mjini Kinsasa, wakilalamika kwa kiongozi huyo anashindwa kutekeleza ahadi aliotoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu.

Changamoto kubwa iliyomkabili Tchisekedi tangu wakati alipoingia uongozini ni kutathmini vipi anaweza kuleta amani kwa taifa hilo hususan eneo la mashariki ambako kumeshuhudiwa ghasia na umwagikaji damu mkubwa wa raia, na uwepo wa wanamgambo waliojihami wanaotekeleza mashambulio.

Maelfu ya watu wamelazamika kuyatoroka mapigano na kuyacha makaazi na mali zao. Na hata kwa waliosalia, wanaishi maisha wakihofia usalama yao.

Haki miliki ya picha
BBC/Mbelechi Msochi

Raia mmoja mwenye umri wa miaka 32, ambaye baba yake aliuwa anaeleza uchungu wa uovu uliowakabili.

‘Tumeomba Felix Tshikedi rais wa Congo atusaidie tumeteseka huko Beni, kila siku watu wauawa, tunaandamana kwa sababu wandugu wetu wamekufa, watoto wamebaki wayatima, rais alifika huko alisema

atamaliza vita lakini hakufanya kitu, tumesema masiku amesha fanya madarakani amesha fanya nini?

‘Hatuta toka hapa tutalala hapa siku tatu.’

Haki miliki ya picha
BBC/Mbelechi Msochi

Raia walioandamana walisindikizwa na baadhi ya wabunge waliochaguliwa wa kutoka Beni hukomashariki mwa nchi.

Wabunge hao wanasema, kuna ripoti ambayo waliwaandikia vyongozi wa nchi kuhusu hali hiyo lakini mpaka sasa ripoti hizo ‘zinafichwa ndani ya kabati za ofisi’.

‘Wanabunge wa muhula uliopita walishuka huko Beni kuangalia nini kilichosabisha vita huko. Waliaandika ripoti yao na kuelezea wazi nini kimepitiakana huko lakini hadi sasa swali hilo hawaja lizungumzia katika baraza la bunge, ripoti imefichwa’ anasema mbunge Katembo Mbusa,

‘Watu wamepeleka habari za uongo ya kwamba ni raia wenyewe ndio wameuwana , ni uongo’ ameongeza mbunge huyo.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Ripoti iliyotolewa Jumatano Agosti 14 na Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch inaeleza kwamba watu 1900 waliuawa, na wengine elfu tatu na mia tatu walitekwa nyara na vikundi vya watu walio na silaha katikati ya Juni 2017 na Juni 2019.

“Zaidi ya makundi 130 yaliojihami yanapigana kwa sababu tofauti katika majimbo ya mashariki Kivu na kulifanya eneo hilo kuwa mojawapo ya yanayotokota zaidi duniani,” amesema Lewis Mudge, Mkurugenzi wa Afrika ya kati kutoka Human Rights Watch.

“Kuelewa nani anayetekeleza uhalifu huu ni hatua ya kwanza ya kuwawajibisha waliohusika na kusitisha uhalifu huo.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *