Maandamano Malawi: Polisi apigwa mawe hadi kufa


Polisi wamekuwa wakikabiliana na waandamanajimjini malawi

Haki miliki ya picha
AFP

Maafisa wa polisi nchini Malawi wamemtaja afisa aliyeuawa siku ya Jumanne wakati wa ghasia za maandamano dhidi ya serikali huko Msundwe – eneo la biashara magharibi mwa mji mkuu wa Lilongwe.

Msemaji wa polisi James Kadadzerab aliambia kitengo cha habari cha AFP kwamba afisa huyo kwa jina Usumani Imedi alipigwa mawe hadi kufa na waandamanaji pamoja na wahalifu.

Ni miongoni mwa maafisa waliowavamia waandamanaji ambao walikuwa wamefunga barabara katika eneo la Msundwe , eneo la upinzani , ili kuwazuia wafuasi wa rais Peter Mutharika kutohudhuria mkutano wake wa kwanza wa kisiasa katika mji huo tangu ushindi wake wa uchaguzi uliokumbwa na utata mwezi Mei.

Wafuasi wa upinzani wamekasirishwa na jinsi tume ya uchaguzi ilivyosimamia uchaguzi huo, ikidai kwamba ulikumbwa na udanganyifu.

Waziri wa maswala ya ndani Nicholas Dausi alisema kwamba watumiaji wengine wa barabara waliwataka maafisa wa polisi kuingilia kati baada ya waandamanji kufunga barabara hiyo inayotumika sana.

Wakati maafisa wa polisi walipowasili , walianza kuwapiga mawe kufikia kiwango cha kupoteza afisa mmoja wa polisi.

Maafisa wa Polisi walirusha vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji lakini wakaendelea kujikusanya kabla ya kurusha mawe….na katika ghasia hizo walimkamata afisa mmoja na kumpiga mawe hadi kufa, shahidi mmoja aliambia AFP.

Takriban watu 12 wamekamatwa na wengine wengi huenda wakazuiliwa , kulingana na gazeti la Nation nchini humo.

Rais Mutharika baadaye alifanya mkutano katika mji mkuu na kuomba utulivu nchini humo , akisema: Hili ni taifa letu tusilichome.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *