Maandamano ya Bobi Wine: 'Polisi wana haki ya kukuua' Uganda


Wafuasi wa mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, walibeba mabango na kuandamana katika maeneo tofauti ya Uganda kupinga hatua ya kukamatwa kwake mapema wiki hii

Maelezo ya picha,

Waandamanaji walikusanya na kuchoma tairi za magari katika mji mkuu wa Kampala, mapema wiki hii

Polisi nchini Uganda wana haki ya kuua kwa kupiga risasi ikiwa “kiwango fulani cha ghasia kitafikiwa”, Waziri wa Usalama Elly Tumwine amesema.

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yalisababishwa na hatua ya kukamatwa kwa mgombea urais wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine yalisababisha vifo vya watu 38 tangu Jumatano wiki hii.

Alishtakiwa kwa kukiuka kanuni za afya za kudhibiti kueneoa kwa virusi vya corona katika mkutano wa kampeni.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema hatua ya kukamatwa ma kushitakiwa kwa Bobi wine ni kisingizio cha kukandamiza upinzani kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Januari.

Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, ni miongoni mwa wagombea 11 wanaopinga rais Yoweri Museveni, ambaye amekewa madarakani tango mwaka 1986.

Bobi Wine aliachiwa kwa dhamana siku ya Ijumaa baada ya kufikishwa mahakamani.

Kukamatwa kwake kulizua maandamano ya vurugo miongoni mwa wafuasi wake. Kundi la vijana lilifunga barabara na kuchoma tairi za magari katika ya mji mkuu wa Kampala, na miji mingine nchini Uganda.

Vikosi vya usalama vilijibu kwa kurusha vitoa machozi na kutumia risasi halisi kuwatawanya watu.

Akiashiria kuwa maafisa 11 wa usalama walijeruhiwa Bw.Tumwine aliwaambia wanahabari kuwa “polisi wana haki ya kukupiga risasi na kukuua ukifikia kiwango fulani cha ghasia”.

“Wataka nirudie? Polisi wana haki ya kukupiga risasi na kukuua na utakufa bur…. usiseme hukuambiwa .”

Katika taarifa, polisi ilisema ni watu 28 waliofarika katika maandamano ya siku ya Jumatano na Alhamisi, lakini shirika la habari AP limemnukuu mchunguzi wa maiti wa polisi na mkuu wa huduma za afya za polisi kwamba walihesabu miili 37 Alhamisi asubuhi.

Maelezo ya video,

Kura za vijana zinaweza kumpa ushindi Bobi Wine?

Mnamo mwezi Juni Bobi Wine aliapa kukiuka marufuku ya mikutano ya kampeni wakati wa janga la corona. Alimshtumu Rais Museveni kwa “kuogopa watu”.

Msmaji wa serikali ya Uganda Don Wanyama ameambia BBC kuwa maafisa “hawengeweza kutualia na kuangalia ghasia kufanyika j”.

Pia amesema RaiS Museveni “ametii marufuku iliyowekwa na Tume ya Uchaguzi na Wizara ya Afya”.

Human Rights Watch linasema ni wazi kwamba mamlaka za Ugandan zinatumia mwongozo wakuzuia Covid-19 kukandamiza upinzani na kuongeza kuwa chama tawala kimefanya kampeni kubwa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *