Mabadiliko ya hali ya hewa: Mkutano wa COP25 waanza kwa wito wa kufikiwa haraka maazimio muhimu


Kutoka kushoto, Waziri wa Uhispania wa kipindi cha mpito wa ekolojia,Teresa Ribera, Rais wa COP Carolina Schmidt na Mkuu wa masuala ya mabadiliko ya haliya hewa katika Umoja wa Mataifa Patricia Espinosa

Haki miliki ya picha
COP25

Image caption

Kongamano la COP25 mwaka huu litaendeshwa na wanawake watatu: Waziri wa Uhispania wa ekolojia kipindi cha mpitoTeresa Ribera, Rais wa COP Carolina Schmidt ana Mkuu wa masuala ya mabadiliko ya haliya hewa katika Umoja wa Mataifa Patricia Espinosa

Viongozi wa kisiasa ma wanadilpomasia wa masuala ya hali ya hewa wanakutana huko Madrid kwa wiki mbili huku mabadiliko ya hali ya hewa yikiendelea kuwa tete.

Viongozi hao wanakutana katika mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa mwaka 2019 maarufu kama COP25.

Kulingana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres bado mabadiliko yanaweza kufikiwa huku Shirika la kimataifa la Save the children likisema kuwa athari za mabadiliko hayo zimeacha mamilioni ya watu wakikumbwa na baa la njaa.

Shirika hilo limeongeza kuwa watu milioni 33 wanahitaji msaada wa dharura kwa sababu ya ukosefu wa chakula cha kutosha kuliko sabbaishwa na vibunga na kiangazi.

COP25 ni nini?

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Maandamano shuleni ni miongoni mwa juhudi zilizofanywa kupigania utunzaji wa mazingira

Mkutano huu ulikuwa umepangiwa kufanyika Chile lakini ukafutiliwa mbali na serikali baada ya maandamano kutokea kwa wiki kadhaa.

Uhispania ilijitokeza kama mwokozi wao na kuamua kuwa mwenyeji wa mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi 29,000 katika kipindi cha wiki mbili.

Akizungumza kabla ya mkutano huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mizozo inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa iko wazi na viongozi wa kisiasa hawana budi zaidi ya kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Mkutano huu unalenga kufikia nini?

Haki miliki ya picha
Save the Children

Image caption

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa zimeathiri nchi nyingi za Afrika, Save the Children linasema, kama huyo mtoto aliye athiriwa vibaya na ukosefu wa lishe bora katika eneo la Mandera, Kenya

“Ni muhimu sana kufikiwa kwa maazimio ya kitaifa katika kipindi cha miezi 12 ijayo tena kwa haraka hasa kutoka kwa nchi zinazotowa kiwango kikubwa cha hewa chafuzi ili kuwezesha kufikiwa kwa dunia isiyokuwa na hewa chafuzi ifikapo mwaka 2050.

“Hatuna budi zaidi ya kusitisha shughuli za uchimbaji na kutumia njia mbadala za uzalishaji wa nishati kwa njia zengine za asilia,”Bwana Guterres amesema.

Karibia kila nchi duniani kwa sasa imetia saini na kuidhinisha makubaliano ya hali ya hewa ya Paris ambapo kila nchi itahitajika kutoa ahadi zake mpya kabla ya mwisho wa mwaka 2020.

Mkutano huu wa Madrid unaashiria kuanza kwa majadiliano yatakayofanyika kwa miezi 12 na kufikia ukomo huko Glasgow kabla ya kuanza kwa mkutano wa COP26 Novemba mwaka ujao.

Je ni nani atakayehudhuria mkutano huo?

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anasema hakuna kituo kipya cha mkaa wa mawe kinahitajiwa kujengwa baada ya mwaka 2020

Viongozi wa dunia karibia 50 wanatarajiwa kuhudhuria mkutao huo utakaofanyika katika mji mkuu wa Uhispania lakini Rais wa Marekani Donald Trump hatakuwepo.

Hata hivyo, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi pamoja na wajumbe wa Bunge la Congress wanatarajiwa kuhudhuria.

Huku uwepo wa Pelosi ukifurahiwa na wengi, wanamazingira wa Marekani wanataka kuona hatua madhubuti juu ya mabadiliko ya hali ya hewa zimechukuliwa.

“Japo ni vizuri kuona kwamba Pelosi anahudhuria mkutano wa Madrid badala ya Trump, kinachohitajika ni kuona hatua za vitendo zimechukuliwa”, amesema Jean Su, kutoka kituo cha Marekani cha Bilolojia Anuai.

“Marekani inasalia katika historia kutokana na mchango wake katika masuala ya kutunza mazingira.”

Madhumuni ya mkutano huu ni yapi?

Haki miliki ya picha
Save the Children

Image caption

Wanyama waliokufa kutokana na ukame nchini Kenya

Shirika la Kimataifa la Save the children linasema kwamba, mafuriko, maporomoko ya ardhi na vimbunga kumesababisha watu milioni 33 kuhitaji msaada wa dharura kwa ukosefu wa chakula cha kutosha huku zaidi ya nusu ya idadi hii ikiaminika kuwa watoto.

Hali hii imekuwa mbaya zaidi kwasababu vimbunga ambavyo vinasemekana kuwa vibaya zaidi vilikumba bara Afrika na kuathiri eneo hilo hilo hiyo ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Kimbunga Idai kilikumba Msumbiji, Zimbambwe na Malawi mwezi Machi, na wiki sita tu baadaye, kimbunga Kenneth kikakumba Msumbiji na mamilioni ya watu wakaathiriwa na mafuriko.

“Mizozo inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa inaendelea kwa sasa na kusababisha vifo, jambo ambalo limewalazimisha kuhama makazi yao na kutatiza hatma ya baadaye ya watoto,” Ian Vale kutoka Shirika la Save the Children amesema.

Unaweza pia kusoma:

“Hali za dharura kama hizi zinaendelea kutatiza mfumo wa misaada ya kibinadamu hadi katika hatua ya kutoweza kudhibitiwa tena. Utokeaji wa vimbunga kunako pelekea ukosefu wa chakula kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa, kunasababisha pengo kubwa kati ya ufadhili na ufikiaji na mahitaji wa misaada ya kibinadamu ambayo hayajatimizwa. Tunakaribia kufikia hali ya hatari katika eneo hili.”

Nini kinatarajiwa kutoka?

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ataambia mkutano huo kwamba, kwa sasa dunia inakabiliana na athari mbaya zaidi zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Pia atahimiza mataifa mbalimbali kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa kiwango kikubwa.

Bwana Guterres amesema ruzuku kwa vyanzo vya nishati ya kaboni vinastahili kusitishwa, na kuongeza kwamba mitambo ya uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe inastahili kujengwa baada ya mwaka 2020.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *