'Mabaki ya kushangaza ya binadamu wa kale yafichuliwa


Sokwe huyo huenda alikuwa hivi

Haki miliki ya picha
Velizar Simeonovski

Image caption

Sokwe huyo huenda alikuwa hivi

Mabaki ya mapya ya sokwe kale yaliyopatikana huenda yakafichua jinsi watu walivyoanza kutembea kwa miguu miwili.

Uwezo wa kutembea kunahusishwa na binadamu.

Mikono yake ilimwezesha kuning’inia juu ya miti,lakini na miguu ya binadamu.

Huenda ilitembea katika matagaa ya miti au hata ardhini kwa miaka milioni 12 zilizopita, wanasayansi wanasema.

Mpaka sasa ushahidi wa kwanza wa sokwe mtu anayetembea wima ulianza miaka milioni sita iliyopita.

Mpaka sasa jinsi ushahidi wa mabaki ya awali yamebaini kuwa mtu alianza kutembea kwa miaka miwili karibu miaka milioni sita iliyopita.

mabaki ya binadamu wanne wa kale – wa kiume na wa kike wawili na mtoto – ilifukuliwa katika shimo lakatika eneo la Bavaria kati ya mwaka 2015 na 2018.

“Mabaki hayo yalipatikana Ujerumani kusini ni hatua muhimu katika kuelewa historia ya uhusiano kati ya binadamu na sokwe mtu, anasema Profesa Madelaine Böhme kutoka chuo kikuu cha Tübingen, Ujerumani.

Alisema nyani huenda wakawa mfano mzuri wa kutegua “kitendaliwi” kati ya binadamu na wanyama hao.

Uvumbuzi huu unatuambia nini kuhusu namna ya kutembea kulivyobadilika?

Tangu zama za Charles Darwin,kumekuwa na mjadala mkali kuhusu jinsi mababu zetu wa kale walivyoanza kutembea kwa miguu miwili.

Haki miliki ya picha
Christoph Jäckle

Image caption

Mifupa ya mkono ya nyani wa kiume Danuvius

Je tabia hii muhimu ya binadamu imetokana na sokwe mtu, kama ile ya orangutan, ambao waliishi kwenye miti, au kutokana na mfumo wa utembezi wababadu zetu, ambao walitumia muda mwingi kutembea ardhini, kama nyani?

Utafiti mpya, uliochapishwa katika jarida la Nature, unashiria kuwa uwezo wwetu wa kusimama wima ni huenda ulitokana na kuwa na mababu sawa walioishi ulaya – na wala sio Afrika, kama ilivyodhaniwa awali.

Mabaki ya mifupa ya Danuvius guggenmosi, ambaye aliishi miaka milioni 11.62 iliyopita, yanaashiria kuwa aliweza kutembea wima kwa miguu miwili na pia miguu yote minne akipanda mahali kama sokwe.

Matokeo haya yanaashiria kuwa kutembea kwa miguu miwili kuligeuka kwenye miti zaidi ya miaka milioni 12 iliyopita, alielezea Prof David Begun, mtafiti kutoka chuo kikuu cha Toronto.

Sokwe alikuaje?

Sokwe wa kiume alikuwa na mifupa kamili,ambayo inafanana na nyani wa kisasa wanaofahamika kama bonobos.

Alikuwa na urefu wa mita moja na karibu kilo 31 na wa kike alikuwa na uzani wa kilo 18, chini ya sokwe mtu yeyote wa kale kuwahi kuishi.

Haki miliki ya picha
Christoph Jäckle

Image caption

Mifupa 21 ya fuvu la kichwa iliyokaribia kukamilika ya nyani wa kiume Danuvius

Kuhifadhiwa kwa mifupa ya viungo vya mwili kama vile, mifupa midogo inayounganisha uti wa mgongo, kidole, mfupa wa kidole cha mguu kulisaidia, watafiti kujenga hoja mpya kuhusu jinsi mnyama alivyotembea.

“Tumefanikiwa kuchunguza jinsi sehemu kadhaa zinazounganisha mifupa inavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na kiwiko cha mkono, paja, goti na kifundo cha mguu, katika mfupa mmoja wa zamani wa siku hizi,” alisema Prof Böhme. “Ilikuwa jambo la kushangaza kubaini jinsi baadhi ya mifupa ilivyofanana na ya mwanadamu, tofauti na sokwe wa jadi.”

Muonekano na mwenendo wa sokwe ni vitu vya kipekee ukilinganisha na wanayama wengine. Kuelewa jinsi tulivyoanza kutembea kwa miguu miwili ni kunaahidi kujibu maswali mengi muhimu kuhusu jinsi spishi zetu zilivyobadilika.

Kutembea wima ilikuwa hatua muhimu katika mabadiliko ya wanadamu, kufungua fursa za kugusa, kuchunguza, na kujifunza jinsi ya kubeba na kutumia vitu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *