Mahakama ya juu DRC yawavua nyadhifa wabunge 20 wa upinzani


Wafuasi wa vyama vya upinzani mkoani Kivu Kaskazini wamegadhabishwa na hatua ya mahakama kuu kikatiba nchini DRC kuwavua nyadhifa zao, wabunge 20 wa upinzani na nafasi zao kupewa wanachama wa muungano wa vyama vya FCC unaoongozwa na rais wa zamani Joseph Kabila. 

Akaizingumza na DW kiongozi wa vyama vya muungano wa Ansemble wake Moise Katumbi mkoani Kivu kaskazini, Muhindo Nzangi, amebainisha kwamba kuondolewa kwa wabunge wao 12, ni alama ya ukandamizwaji wa demokrasia inchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 

Mawakala wa vyama vya upinzani wameinyooshea kidole cha lawama mahakama kuu ya kikatiba kwa kula njama ili kuwapa nafasi wabunge kutoka muungano wa vyama vya FCC unaoongozwa na Rais wa zamani Joseph Kabila ambaye hadi sasa anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika utawala wa sasa.

Rais wa zamani Joseph Kabila angali ana ushawishi nchini DRC

Rais wa zamani Joseph Kabila angali ana ushawishi nchini DRC

Katika tangazo lake kwenye vyombo vya habari, katibu mkuu wa chama cha MLC chake Jean Pierre Bemba, bibi Eve Bazaiba, amesema maandamano makali yateaendeshwa Jumamosi tarehe 15 Juni kote nchini ili kuomba ukweli wa uchaguzi uliopita uliompa Rais Felix Tshisekedi ushindi.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi kuzuiliwa kuwasili mjini Goma hali ambayo imesababisha wafuasi wake kupoteza matumaini yao kwa utawala wa sasa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *