Mahojiano ya Oprah: Mke wa mwanamfalme Harry , Meghan Markle 'hakutka kuwa hai'


Meghan Markle

Mke wa mwanamfalme huyo, Meghan Markle amesema wakati mwingine alipata maisha kuwa magumu sana katika familia ya kifalme na ‘hakutaka tena kuwa hai’Katika mahojiano ya kibinafsi na yenye hisia kali ya runinga, Meghan alimuambia Oprah Winfrey kwamba hakupata usaidizi wakati alipouitisha .

Amesema kibaya zaidi ilikuwa wakati mtu mmoja wa familia hiyo alipomuuliza Harry jinsi mtoto watakayemzaa atakuwa na ‘ngozi nyeusi’ .

Prince Harry pia alifichua kwamba babake Prince Charles aliacha kuzipokea simu zake alipogundua kwamba alikuwa na mpango wa kujiondoa kutoka familia ya kifalme .Mahojiano hayo na Oprah yaliongojewa sana yalipeperushwa usiku nchini Marekani Wakati wa mahojiano hayo maalum ya CBS ya saa mbili ambayo yatapeperushwa siku ya jumatatu saa tatu usiku katika runinga ya ITV nchini Uingereza na pia kwenye ITV Hub kwa hisani ya Harpo Productions/CBS, wawili hao wamezungumzia masuala mbali mbali ikiwemo ubaguzi wa rangi ,uhusiano wao na vyombo vya habari ,afya ya kiakili na mambo katika familia ya kifalme.Pia walitangaza kwamba mtoto wanayemtarajia hivi karibuni ni msichana.

Wawili hao walihamia Carlifornia baada ya kujitoa kutoka majukumu ya familia ya kifalme Machi mwaka wa 2020 na ilitangazwa mwezi jana kwamba hawatarejea kama wanachama wa familia ya kifalme .Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *