Mamia ya tembo wafariki Botswana


Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika ina idadi kubwa kabisa ya wanyamapori, ikadiriwa kuwa 130,000. Cyril Taolo, kaimu mkurugenzi mkuu wa Idara ya Wanyamapori na Mbuga za Kitaifa amesema wana ripoti ya vifo vya ndovu 356 katika eneo la kaskazini mwa Okavango Delta na wamethibitisha vifo vya tembo 275 mpaka sasa. Amesema chanzo cha vifo hivyo bado kinachunguzwa. Sampuli zimechukuliwa na kutumwa Afrika Kusini, Zimbabwe na Canada kwa ajili ya kupimwa. Vifo kama hivyo vilitokea Mei wakati maafisa walipopata mizoga 12 katika kipindi cha wiki moja kwenye kijiji kimoja cha kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *