Marekani : Maafisa wa CIA na Usalama wa Taifa watoa maelezo ya madai ya hujuma za Russia kwa viongozi wa wabungeIkulu ya Marekani White House imethibitisha kwamba Mkurungenzi wa Idara ya Ujasusi,CIA, Gina Haspel na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Paul Nakasone, watakutana na kundi la wabunge wanaojulikana kama Gang of Eight.

Mkutano huo utawapa fursa ya kwanza wabunge kusikiliza maelezo moja kwa moja kutoka kwa maafisa wa ujasusi waliobobea juu ya madai hayo.

Shirika la habari la Reuters likinukuu vyanzo vya serikali ya Marekani na nchi za Ulaya, vinaripoti kwamba Marekani hivi karibuni ilipata ripoti ya ujasusi ambayo inathibitisha madai hayo ya Russia kutoa pesa na vifaa vya kijeshi kwa Taliban ili kushambulia wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa jeshi la ushirika.

Lakini Trump amekanusha madai hayo, na jana aliandika kwenye ukurusa wake wa Twitter kwamba habari hiyo ya mpango wa Russia kuwaua wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan ni uzushi.

Kwa upande wao maafisa wa kundi la Taliban nao wamejitokeza na kuthibitisha mpango huo.

Kamanda wa Taliban Ghazni Moulani Baghdadi ameliambia gazeti la Business Insider kwamba, makamanda wa Taliban wamekuwa wakipokea pesa na vifaa vya kijeshi kutoka kwa idara ya ujasusi ya Russia.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *