Marekani yaadhimisha 9/11Rais Donald Trump alihutubia jamaa na marafiki wa waathiriwa wa mashambulizi hayo kwenye hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kijeshi na wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon.

Trump alisema kuwa Marekani kamwe haitasahau mashambulizi hayo ya kigaidi.

Rais huyo, ambaye alikuwa ameandamana na mkewe, Melania Trump, aidha alisema matukio hayo ya mwaka 2001 yaliwapa ujasirizidi raia wa Marekani.

Rais wa zamani wa Marekani, George W Bush, ni kati ya viongozi walioweka shada la maua katika sehemu maalum ya kumbukumbu ya waliopoteza maisha yao siku hiyo nje ya majengo ya Pentagon. Bush ndiye aliyekuwa kiongozi wa Marekani wakati wa mashambulizi hayo.

Mjini New York, majina ya watu waliouawa wakati wa mashambulizi hayo, yalisomwa, katika hafla iliyofanyika kwenye bustani maarufu kama “Ground Zero.”

Makamu wa Rais, Mike Pence, aliongoza hafla iliyofanyika mjini Shanksville, Penslvania, karibu na mahali ambapo Ndege ya United Airlines, ilianguka baada ya abiria kukabiliana na magaidi waliokuwa wameiteka, wakiwa na nia ya kushambulia ikulu ya Marekani hapa mjini Washington DC.

Haya yalijiri siku chache baada ya Rais Trump kutangaza kwamba alikuwa amefuta mwaliko aliokuwa ametoa kwa viongozi wa kundi la wanamgambo wa Taliban, kuzuru Marekani kwa mazungumzo ya kutafuta anmani nchini Afghanistan.

Taliba ilishutumiwa kuhusika kwa njia moja au nyingine, na mashambulizi hayo.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha New York, David Monda, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba Marekani sasa imetambua kwamba haiwezi kutokomeza ugaidi kwa kutumia zena za kijeshi.

Hata hivyo, Monda alisema kuwa licha ya hali ya kulinda usalama kwendelea kuimarishwa katika viwanja mbalimbali vya ndege, bado kuna wasiwasi kuhusu ugaidi kwingineko duniani.

“Ingawa hapa Marekani takwimu zinaonyesha kwamba ugaidi umepungua, bado kuna maeneo mengine duniani ambayo yanaendelea kuathiriwa mno na vitendo vya ugaidi,” alisema.

Mashambulizi hayo yalibadilisha kabisa jinsi Marekani inavyotzazama ugaidi na usalama wa kitaifa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *