Marekani yawaondoa wafanyikazi wake kutoka Iraq huku wasiwasi kati yake na Iran ukiongezeka


Iraq inasema kuwa haijaoona vitendo vinavyoonekana kuwa tishio

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Iraq inasema kuwa haijaoona vitendo vinavyoonekana kuwa tishio

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imeagiza kuondoka kwa kwa wafanyikzi ‘wasiofanya kazi za dharura’ nchini Iraq kufuatia hali ya waiswasi kati ya Marekani na Iran.

Wafanyikazi katika ubalozi mjini Baghdad na wale wa ubalozi wa Irbil wametakiwa kuondoka haraka iwezekanavyo katika uchukuzi wa kibiashara.

Ujerumani wakati huohupo imesitisha mafunzo ya wanajeshi wake nchini Iraq.

Jeshi la Marekani lilisema siku ya Jumanne kwamba kiwango cha vitisho hivyo mashariki ya kati vilitolewa kutokana na ujasusi kuhusu vikosi vinavyoungwa mkono na Iran katika eneo hilo.

Ni kinyume na matamshi ya Jenerali mmoja wa Uingereza aliyesema kuwa hakuna vitisho vyovyote vilivyoongezeka.

Chris Ghika ambaye ni naibu kamanda ya muungano wa majeshi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Islamic State , aliambia maripota kwamba hatua zilizochukuliwa kuwalinda wanajeshi wa Marekani na washirika wao kutokana na vikosi vinavyoungwa mkono na Iran nchini Iraq na Syria zinatosha.

”Tunajua uwepo wao na tunawachunguza pamoja na wengine kwa sababu hayo ndio mazingira tuliopo kwa sasa”, aliongezea.

Lakini msemaji wa jeshi la Marekani baadaye alikanusha matamshi ya jenerali Ghika akisema kuwa yalienda kinyume na vitisho vilivyotambuliwa na Marekani pamoja na mashirika yake ya kijasusi.

Idara ya ulinzi nchini Ujerumani ilisema siku ya Jumatano kwamba jeshi la Ujerumani lilisitisha mipango ya mafunzo yake nchni Iraq.

Msemaji wake alisema kuwa kulikuwa na hali ya tahadhari miongoni mwa wanajeshi wake 160 wanaohusika katika operesheni hiyo.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Marekani inavichukulia vikosi vinavyoungwa mkono na Marekani kuwa tishio kubwa

Mapema, chombo cha habari cha Reuters kilinukuu duru za usalama za Iraq kikisema kwamba wakati wa ziara nchini Iraq mapema mwezi huu waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo aliambia makamanda wa Iraqi kwamba ujasusi unaonyesha kwamba vikozi vinavyoungwa mkono na Iran vilikuwa vikiweka roketi karibu na kambi zinazoishi wanajeshi wa Marekani.

Ujumbe kutoka kwa Marekani ulikuwa wazi. Walitaka kuhakikishiwa kuwa Iraq itayazuia makundi yanayotishia maslahi ya Marekani , mojawapo ya duri hizo ilinukuliwa ikisema.

Ilisema kuwa iwapo Marekani itashambuliwa katika ardhi ya Iraq, itachukua hatua za kujilinda bila ya ushirikiano na Baghdad.

Waziri mkuu nchini Iraq Adel Abdul Mahdi , alisema siku ya Jumanne kwamba vikosi vyake vya usalama havijaona vitendo vya kutilia shaka vinavyotishia upande wowote.

Vikosi vinavyoungwa mkono na Iran vimekuwa na jukumu kubwa katika vita dhidi ya IS nchini Iraq.

Msemaji wa makundi hayo mawili aliambia chombo cha habari cha Reuters kwamba matamshi ya kuwepo kwa vitisho kwa majeshi ya Marekani ni vita vya kisaikolojia.

Marekani haina uwepo wa kidiplomasia nchini Iran.

Ubalozi wa Uswizi unawakilisha maslahi ya Marekani katika taifa hilo.

Pia iliripotiwa siku ya Jumanne kamba wachunguzi wa Marekani wanaamni kwamba Iran ama makundi yake yalitumia vilipuzi kulipua meli nne za mafuta katika pwani ya UAE siku ya Jumapili.

Mashimo makubwa yalipatikana katika maeneo ya chini ya meli hizo lakini hakuna ushahidi uliotolewa kuonyesha kwamba shambulio hilo linahusishwa na Iran.

Mapema mwizi huu , Marekani ilituma meli inayobeba ndege na makombora katika eneo la Ghuba.

Kulikuwa na onyo la mara kwa mara kutoka kwa Washington ambayo ilitaka kutoa sababu zake kuhusu lengo la kupeleka vifaa vyake katika eneo la mashariki ya kati.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *