Mashambulio ya tindikali, jinamizi linalowatia hofu wengi


Flavia Naampima muathiriwa wa shambulio la Tindikali anasema mtizamo wa maisha yake umebadilika baada ya shambulio dhidi yake

Image caption

Flavia Naampima muathiriwa wa shambulio la Tindikali anasema mtizamo wa maisha yake umebadilika baada ya shambulio dhidi yake

Unaposikia taarifa kuhusu hujuma za Acid… yaani watu kumuwagiwa tindikali usoni au Mwili mara nyingi ukatili huu huhusishwa na bara Asia. Hata hivyo kuna visa vingi vya watu kushambuliwa kwa tindikali ambavyo vinaripotiwa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.

Mwandishi wa BBC David Wafula amekuwa nchini Uganda ambapo amekutana na wathiriwa wa hujuma za tindikali.

Mmoja wa waathiriwa ni Flavia Naampima ambaye anasema alishambuliwa alipokuwa nje ya lango la nyumbani kwao alipokuwa akitoka shuleni:” Ilikuwa jioni nilipokuwa nikitoka shule, niliona mtu amesimama kwenye ukuta, nilidhani anasubiri mtu, na hakukuwa na mtu nyumbani”. Alikumbuka Bi Nampima.

”Ghafla nilisikia mtu akitembea nyuma yangu, nilipogeuka, nilimwagiwa kitu nilichofikiria ni maji, baada ya sekunde chache nilihisi kama naungua, nilipiga kelele, nikikimbia hapa na pale, nguo zangu zilianza kuungua, nakaanza kuzirarua nikizitoa mwilini, nilivuta sketi niliyokua nimeoivaa, na kufunika kifua changu, na kutembea hadi kwa jirani…walinipeleka hospitalini na nakumbuka dakatari akisema ‘mbona hamukumwagia maji?, nilimwagiwa maji huku nikilia”. Aliongeza

Baada ya miezi minane hosptalini, Flavia alirejea nyumbani kwa mara ya kwanza, hatua ambayo ilikuwa nzito sana kwake.

Image caption

Flavia Naampima Muathiriwa wa shambulio la Tindikali

Bi Flavia anasema haikuwa rahisi kushuhudia eneo ambalo kisa cha mashambulio kilitokea , akiielezea safari yake ya kurudi nyumbani kama ya mtoto mdogo: ”Kwa kweli ilikuwa ni hatua ndogo baada ya nyingine, ni taswira inayojitokeza kila mara ninapopita hapa”, alisema.

Ni kisa ambacho hatakisahau maishani mwake, kutokana na kwamba kilibadilisha masiha yake na anasema kila siku hupata msukumo wa kukubali kilichomtendekea miaka kumi na moja iliyopita.

”Nilitafuta ile kazi niliyotaka, nikaweka bidii, na ndivyo ndivyo nilivyoamua kuishi maisha yangu, kuna mambo mengine mimi huyafanya kujiburudisha, napenda densi ya aina ya salsa, imenisaidia sana katika safari yangu ya uponaji, kwa mara ya kwanza, nilikuwa muoga, sikudhani kuna mtu ambaye angependa kucheza ngoma na mimi, lakini nilibobea.

Athari za kisakolojia, kiakili na majeraha kutokana na hujuma za tindikali hufanya uponaji kwa manusura kuwa mgumu, kwa baadhi yao hupata changamoto kupata kazi, hivyo hulazimika kutegemea ujuzi walionao kukidhi maisha kama anavyofanya Namuyomba Jamida , anayesuka mikeka.

Image caption

Namuyomba Jamida alikosa kazi ya kufanya na kuamua kusuka mikeka na vikapu baada ya shambulio la tindikali

” Baada ya kushambuliwa kwa tindikali, maisha huwa magumu, nilipoteza kazi yangu kwa hiyo niliamua kuja mjini na hapo nilikutana na manusura wa mashambulio ya tindikali ,na kwa pamoja tukajifunza kujikimu kimaisha. Kila siku nafanya kazi hii kwa ajili ya watoto wangu watano.”

Wanaharaki nchini Uganda wanahamashisha raia kuhusu ukatili huu. Reenah Ntoreinwe kutoka shirika la End Acid Violence Uganda ambalo limewasajiri manusura 350 jijini kampala pekee ana anasema sharia ni hafifu:

“Tindikali nchini Uganda huuzwa kwa bei rahisi sana, na inapatikana kwa urahisi sana, sheria ni dhaifu mno, kununua asidi ni kama kuenda dukani na kukunua ndizi, kikombe kimoja cha asidi kinagharimu chini ya dola 2, nchini Uganda visa vya mashambulio ya tindikali ni vingi kuliko vya bunduki, tunahitaji sheria ambazo zitasaidia watu, hebu tafakari unamwagia mtu kitu ambacho kina uwezo wa kumaliza chuma, je mwili wa mtu??.

kulingana na takwimu katika hospitali moja jijini Kampala, katika muda wa wiki mbili hapakosi mtu aliyeshambuliwa na tindikali , jambo ambalo naibu mkuu wa polisi nchini Uganda Pauline Amaye anasema ni tatizo kubwa.

”Nijambo la kawaida kusikia kesi za iana hii na sit u kampala, pia katika miji mingine nchini, ni jambo la kuhuzunisha kwamba watu hawatafuti njia mbadala za kutatua mizozo, bunge kwa sasa limwasilisha mswada wa kureebisha sharia kuhusu hujuma za asidi.”

Daktari Adan Abdullahi anasema kwamba njia ya uponaji inachukua muda, lakini kwa matibabu yanayofaa mtu anaweza kupona kikamilifu:

Mtu anaposhambuliwa, kwanza kabisa aoshwe na maji mengi kupunguza makali. Amwagiwe maji kwa takriban dakika arobaini na tano…Tumia maji masafi kupunguza kuambukizwa kwa magonjwa kisha mgonjwa akimbizwe hospitalini katika kitengo kinachokabiliana na majeraha ya kuungua, na baada ya majeraha kupona tunaweza kufanya upasuaji wa kupandikiza ngozi upya na kurejesha umbo la muathiriwa karibu na hali ya kawaida, kando na upasuaji, matababu ya kisaikolojia ni muhimu .

Wakati Flavia na Jamida wanaendelea kupona, watu waliowashambulia waathiriwa hawajawahi kubainika na kufikishwa mbele ya sheria, na hadi pale kutakuwa na sharia kali, waathiriwa watazidi kuishi kwa hofu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *