Mashambulizi ya hifadhi za mafuta za Saudia: Marekani yatuma wanajeshi zaidi Saudia kukabili vitisho vya Iran


Wanajeshi hao wanalengo kuimarisha ulinzi wa Saudia

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Wanajeshi hao wanalengo kuimarisha ulinzi wa Saudia

Idara ya ulinzi Pentagon nchini Marekani imetangaza kupelekwa kwa maelfu ya wanajeshi ili kuimarisha ulinzi wa Saudia.

Waziri wa maswala ya ulinzi nchini humo Mark Esper anasema kwamba ameagiza kupelekwa kwa wanajeshi zaidi , ikiwemo ndege za kijeshi na mfumo wa kulinda mashambulizi ya angani.

Amesema kwamba hatua hiyo inalenga kujibu vitisho katika eneo hilo mbali na kuulinda ufalme huo kutoka kwa uchokizi wa Iran.

Hatua hiyo inajiri baada ya mashambulizi dhidi ya hifadhi za mafuta za Saudia mwezi Septemba.

Pamoja na wanajeshi wengine idadi hiyo inajumlisha zaidi ya wanajeshi 3,000 ambao wamepelekwa ama kuruhusiwa kutoka katika kipindi cha mwezi mmoja, alisema msemaji wa Pentagon Jonathan Hoffman.

Marekani imeongeza vikosi vyake katika eneo hilo kufikia wanajeshi 14,000 tangu mwezi Mei, kulingana na CNN.

”Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman ametaka usaidizi zaidi”, alisema bwana Esper.

Shambulio dhidi ya hifadhi za mafuta za Saudia ziliathiri asilimia 5 ya mafuta kote duniani na kusababisha bei za mafuta kupanda .

Zote Saudia na Marekani zinailaumu Iran kwa shambulio hilo.

Mohammed bin Salman alisema: Iwapo ulimwengu hautachukua hatua madhubuti dhidi ya Iran kutakuwa na uchokozi zaidi ambao utatishia maslahi ya ulimwengu.

Iran imekana madai kwamba ilihusika katika shambulio hilo.

Hatahivyo viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza katika taarifa ya pamoja walisema kwamba hakukuwepo maelezo zaidi kuhusu shambulio hilo.

Bwana Esper aliambia wanahabari katika idara hiyo ya ulinzi siku ya Ijumaa kwamba ushahidi kutoka kwa mashambulio hayo ulithibitisha kwamba Iran ndio ya kulaumiwa.

Alisema kwamba tabia hiyo mbaya ni miongoni mwa malengo ya taifa hilo kuyumbisha eneo lote la mashariki ya kati na kuharibu uchumi wa dunia.

” Jaribio la Iran la kutumia ugaidi , vitisho na nguvu za kijeshi ili kuafikia malengo yake ni kinyume na maadili ya kimataifa”, aliongezea Esper.

Saudia ni rafiki wa muda mrefu wa usalama katika eneo la mashariki ya kati na ametaka usaidizi wa wanejshi zaidi ili kuimarisha ulinzi wao na kutetea sheria za kimataifa.

Uchanganuzi wa Gary O’Donoghue, mjini Washington

Utasamehewa kwa kuchanganyikiwa kuhusu tabia ya rais Trump kuhusu upelekeji wa wanjeshi wa Marekani katika eneo la mashariki ya kati.

Wakati mmoja alikuwa akituma ujumbe wa twitter kuhusu matrilioni ya madola ambazo Marekani imepoteza katika vita visivyoisha katika eneo hilo na kuapa kwamba Marekani itajiondoa katika mzoza wa mashariki ya kati.

Na sasa kuna takriban wanajeshi 3,000 zaidi wanaoelekea Saudia na kufanya vikosi hivyo kuongezeka na kufikia 17,000 tangu mwezi Mei.

Rais Trump sio wa kwanza wa ikulu ya Whitehouse kukumbana na presha hiyo ya kukanganya, rais Obama alilazimika kuondoa ahadi yake 2015 ya kuleta pamoja wanajeshi wote wa Marekani , kuzuia baadhi , lakini kufikia sasa kuna takriban wanajeshi 14,000.

Rais Trump mara kwa mara ametetea uhusiano wa Marekani na kiongozi wa Saudia akiutaja ufalme huo kuwa mshirika muhimu ambaye amewekeza sana Marekani.

Lakini wabunge kutoka maeneo yote wamekosoa ufalme huo tangu mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi mbali na kuhusika kwa Saudia katika vita vya Yemen.

Mwezi Juni , bunge la seneti lenye wabunge wengi wa Republican lilionyesha wasiwasi wake kwamba vikosi vya Saudia vitatumia silaha dhidi ya raia nchini Yemen.

Huku Marekani ikijiandaa kutuma wanajeshi zaidi katika ufalme huo, Trump pia amekumbwa na shinikizo kutoka bunge la Congress kwa uamuzi wake wa kuviondoa vikosi vya Marekani nchini Syria.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *