Matokeo ya uchaguzi Marekani: Je Trump anaweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi


Trump at rally

Karibu wiki mbili baada ya Joe Biden kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Marekani, Donald Trump bado hajakubali kushindwa. Je ana mpango wa kubadilisha matokeo hayo?

Mkakati wa rais wa kupinga matokeo ya uchaguzi kisheria unaonekana kugonga mwamba kote nchini. Timu ya Trump bado haijapiga hatua ya maana, au kutoa ushahidi wa kubainisha kura ziliibwa baada ya kuwasilisha kesi kadhaa mahakamani.

Wakili wake mkuu, Maya wa zamani New York City Rudy Giuliani, alisema situ ya Alhamisi kwama kampeni ya Trump itaachana na kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Michigan, ambako Biden alishinda kwa zaidi ya kura 160,000.

Jimbo la Georgia, limeidhinisha rams matokeo ya uchaguzi, ambao umempatia Biden ushindi wa zaidi ya kura 12,000 baada ya kura karibu million tano kuhesabiwa tena kwa mikono.

Huku uwezekano wa kupinga kisheria matokeo ya uchaguzi mahakamani ikielekea kugonga mwamba, rais anaonekana kubadli mkondo katika mbinu ya kugeuza matokeo ya uchaguzi kwa kutumia kamari ya kisiasa.

Mwongozo wa hatua kwa hatua ya mkakati wa Trump

Haya ndio mambo huenda akafanya:

1. Kuzuia mchakato wa kuidhinisha rasmi matokeo ya uchaguzi katika majimbo mengi kadri iweekanavyo, ima kupitia kesi mahakamani au kuwashawishi maafisa wa Republican kupinga

2.Kuwashawishi wabunge katika majimbo yanayoongozwa na Republican ambako Biden alipata ushindi mwembamba kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi kutokana na ufisadi na udanganyifu

3.Bunge lipewe kura ya wajumbe wa jimbo lao, ambayo hupigwa na “wajumbe maalum” Desemba 14, waamue kumpatia Trump Nacala ya Biden

4.Wakifanya hivyo katika majimbo ya – Wisconsin, Michigan na Pennsylvania, kwanza mfano- kumnyanyua Trump kutoka kura 232 za wajumbe alizo nazo sasa hadi kura 269- ambayo itakuwa zaidi ya alama ya ushindi

5.Pia hatua ya kumuondoa Biden kutoka kwa kura 306 huenda ikafanya kazi, kwa sababu hili likitokea uchaguzi utaamuliwa katika Bunge la Wawakilishi, ambalo japo linaongozwa na Democrats, Trump huenda akawa na nafasi ya kushinda kutokana na baadhi ya sheria ambazo zinaeleweka na watu wachache

Trump anafanya nini kufanikisha mkakati huu?

Anatumia shinikizo kwa watu ambao huenda wakabadilisha ni nani majimbo yanaweza kumchagua rais.

Wamarekani wanaposhiriki uchaguzi wa urais, huwa ni uchaguzi wa mashindano ya majimbo sio ya kitaifa. Wanawapigia kura wajumbe maalum wa ambao wanampigia rais kura moja kila mmoja wao. Hao wajumbe hufuata uamuzi wa wapiga kura – katika jimbo la Michigan, kwa mfano, wote wanatakiwa kupigia kura Joe Biden kwasababu ameshinda uchaguzi katika jimbo hilo.

Siku ya Jumatatu, bodi ya jimbo hilo inayojumuisha Warepublican wawili na Wademocrats wawili wanatarajiwa kukutana kuhesabu kura na kuthibitisha rasmi kuwa kura 16 za wajumbe zinamwendea Biden.

Fununu ya kwanza kuashiria Trump anashinikiza majimbo husika kupuuzilia mbali matokeo ya uchaguzi ilidhihirika kufuatia ripoti kwamba aliwaalika White House maafisa wa Republican ambao awali walikataa kuthibitisha matokeo ya uchaguzi kutoka mji wa Detroit ambao ni mkubwa katika jimbo la Michigan.

Fununu hizo zilibainika baada ya baada ya viongozi wa Republican katika bunge la Michigan kukubali mwaliko wa rais kuzuru White House siku ya Ijumaa.

Je Hali kama hii ishawahi kutokea?

Mara ya mwisho uchaguzi ulikuwa na ushindani wa karibu ilikuwa mwaka 2000 kati ya Al Gore na George W Bush. Kulikuwa na ushindani mkali katika jimbo la Florida,ambako tofauti ya kura kati ya wagombea ilikuwa kura mia kadhaa. Hatimaye mMahakama ya Juu zaikai ya Marekani iliingilia kati na kusimamisha ukaguzi zaidi – na Bush akawa rais.

Katika uchaguzi ambao matokeo katika majimbo kadhaa yamekumbwa na utata ni ule wa mwka 1876 kinyang’anyiro kati ya Rutherford B Hayes wa Republican na Samuel Tildon wa Democratic.

Katika uchaguzi huo, matokeo yaliyopingwa ni ya Louisiana, South Carolina na Florida kumaanisha hakuna mgombea aliyeweza kushinda kura ya wajumbe.

Mkwamo huo uliwasilishwa mbele ya Bunge la Wawakilishi la Mraekani, ambalo lilimuunga mkono Hayes, ambayo ilikuwa kama Bush mwaka 2000 na Trump mwaka 2016, ambao walishinda kwa kura chache kitaifa kuliko za mpinzani aliyeshindwa.

Nini kitatokea ikiwa Donald Trump atakataa kuondoka ofisini?

Ikiwa jaribio la Trump kubadili matokeo ya uchaguzi litagonga mwamba, Januari 20 sea Sita na dakika moja Joe Biden ataapishwa kuwa rais wa 46 wa Marekani hata kama Trump atakuwa amekubali rasmi kushindwa au la.

Wakati huo, wahudumu wa ulinzi wa kisiri na majeshi ya Marekani watakawu huru kumchukulia hatua rais wa zamani kama wanavyofanyia watu ambao hawajaidhinishwa kuingia majengo ya serikali.

“Anachofanya kinashangaza sana,” Biden alisema katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Alhamisi. “Ujumbe unaopokelewa kote duniani kuhusudemokrasia inavyofanya kazi ni mbaya sana.”

Hata kama rais hatafanikiwa katka jitihada jizo, hatua aliyochukua imeweka mfano kwa chaguzi zingine zijazo ana kulingana na kura za maoni anahujumu imani ya Wamarekani katika mfumo wa demokrasia na taasisi zingine za kikatiba.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *