

Raia wa Uganda hii leo wanashiriki katika shughuli ya kihistoria ya kumchagua rais na wawakilishi wa bunge lao .
BBCSwahili itaendelea kukupataia matangazo mubashara ya matokeo hayo kuanzia jioni hii leo punde tu shughuli ya kupiga kura itakapokamilika.
Matokeo ya maeneo bunge yataanza kutangazwa muda tu baada ya shughuli ya upigaji kura kukamilika huku yale ya urais yakitarajiwa siku chache zijazo.
Wakati huohuo Shughuli ya kupiga kura ilianza mwendo wa saa moja alfajiri licha ya kwamba baadhi ya maeneo yalikuwa hayajapata vifaa vya kupigia kura.
Hatua hiyo inajiri baada ya Intaneti kuminywa saa chache kabla ya uchaguzi huo kuanza.
Bobi Wine ndiye wa kwanza kuthibitishwa kupiga kura katika eneo la Freedom Square.
Mapema leo Milolongo mirefu ilishuhudiwa katika vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini Uganda.
Raia waliokuwa na hamu ya kupiga kura walifika katika vituo hivyo mapema zaidi kabla ya vituo hivyo kufunguliwa huku wakionekana kuwa na hamu ya kushiriki katika shughuli hiyo ya kihistoria.