Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020: Juhudi za timu ya Trump za kupinga matokeo ya Pennsylvania zagonga mwamba


Marekani
Maelezo ya picha,

Rais wa Marekani Donald Trump

Mahakama moja huko Pennsylvania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na timu ya Trump inayopinga matokeo ya uchaguzi ambayo ilikuwa inataka kura zilizopigwa kwa njia ya posta katika jimbo hilo zifutiliwe mbali.

Jaji Matthew Brann alisema kesi hiyo ambayo imeegemea wizi wa kura haikuwa na “msingi wowote”.

Hatua hiyo inawezesha rais mteule kuidhinishwa kuwa mshindi wa jimbo la Pennsylvania wiki ijayo ambaye anaongoza kwa zaidi ya kura 80,000.

Hili ndio pigo la hivi karibuni kwa Donald Trump ambaye anajaribu kupinga matokeo yanayoonesha kuwa alishindwa katika uchaguzi mkuu wa Novemba 3.

Bwana Trump amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na wizi wa kura bila ya kutoa ushahidi wowote.

Bwana Biden anakadiriwa kumshinda Rais Donald Trump kwa kura 306 dhidi ya 232 za wajumbe ambazo ndio huamua nani anakuwa rais wa Marekani.

Kampeni ya Trump imepoteza kesi kadhaa ilizowasilisha kupinga matokeo ya uchaguzi na juhudi zao za hivi karibuni zimekuwa kusitisha majimbo muhimu kumuidha Biden wa chama cha Democrat mshindi.

Uamuzi wa Jaji Pennsylvania

Kampeni ya Trump ilisema kuwa jimbo hilo limekiuka katiba ya Marekani inayolinda pande zote kwa madai kuwa wapiga kura wa Democratic waliruhusiwa kurekebisha makosa waliofanya katika kura zao huku wale wa chama cha Republican wakinyimwa fursa hiyo.

Hata hivyo Jaji Brann alitupilia mbali madai hayo na kusema kuwa hata kama timu ya Trump ilikuwa inatafuta msingi wa kesi wazilowasilisha, timu hiyo ilivuka mpaka wakati wanatafuta suluhisho.

Baadhi ya wana Republican watoa wito kwa rais Trump kukubali kuwa ameshindwa lakini baada ya hakimu wa Pennsylvania kutoa uamuzi wake, Seneta wa jimbo hilo wa chama cha Republican amesema sasa Trump amemaliza njia alizokuwa nazo kupinga matokeo ya uchaguzi na kumsihi akubali matokeo.

Hata hivyo, Wakili binafsi wa Trump, Rudy Giuliani, amesema katika taarifa atapinga uamuzi huo: “Uamuzi wa leo unaonekana kusaidia katika mkakati wetu wa kuwasilisha kesi yetu katika mahakama ya juu zaidi.”

Hali ikoje katika majimbo mengine?

Jumamosi, timu ya kampeni ya Trump ilitaka kura za Georgia, zihesabiwe tena siku moja baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura zilizohesabiwa tena za eneo hilo moja baada ya nyingine kwa mkono na Bwana Biden kuthibitishwa mshindi wa jimbo hilo.

Katika jimbo jingine ambalo yeyote kati ya wagombea wa urais alikuwa na uwezo wa kushinda la Michigan, maafisa wa Republican waliandikia bodi ya uchaguzi ya jimbo hilo kuomba kuidhinishwa mshindi wa jimbo hilo kucheleweshwa kwa wiki mbili.

Timu hiyo ilitaka kura za rais kuhesabiwa tena katika kaunti kubwa ya Detroit na kupinga rasmi matokeo hayo.

Hata hivyo idara maalum ya Michigan ilisema kuchelewesha kuidhinishwa kwa mshindi hakuruhusiwi kisheria.

Katika jimbo la Wisconsin, maafisa wa uchaguzi waliwashutumu wafuasi wa Trump kwa kutatiza shughuli ya kuhesibiwa tena kwa kura.

Walisema kuwa waangalizi wa Bwana Trump kuna wakati walikuwa wanapinga kila kura ili kuchelewesha kimaksudi mchakato huo.

Ikiwa shughuli ya kura kuhesabiwa tena haitakuwa imekamilika kufikia Desemba 1 – siku ya mwisho ya jimbo la Wisconsin kumuidhinisha mshindi – timu ya Trump itakuwa na uwezo wa kuendelea na mchakato wa kupinga matokeo kisheria.

Maelezo ya video,

Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Tazama Trump alivyodai kura ‘zimeibiwa’Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *