Mbappe alinganishwa na Pele katika historia ya ufungaji magoli duniani


Kylina Mbappe

Haki miliki ya picha
Getty Images

Huku akifunga goli lake la 100 dhidi ya Andorra siku ya Jumanne, Kylian Mbappe aliweka rekodi ya kuwa mfungaji wa mabao mengi duniani akiwa na umri wa miaka 20.

Ni wachezaji wachache katika historia ya soka waliofunga idadi hiyo ya mabao kabla ya kufikisha miaka 21.

Messi na Christiano Ronaldo hawakuweza kufunga idadi hiyo ya magoli wakiwa na umri kama huo.

Rekodi hiyo mpya inampatia Mbappe utofauti mkubwa ikilinganishwa na wachezaji wengine katika historia ya soka.

Akiwa na umri wa miaka 20 , ufanisi wa Kylian Mbappe umewawacha wengi wakienzi kipaji chake.

Kylian Mbappe aliifungia AS Monaco magoli 27, tayari ameifungia PSG magoili 60 na hivi majuzi aliifungia timu yake ya taifa goli la 13.

Mbali na hayo Mbappe ametoa usaidizi wa magoli mara 58 katika mechi 180 alizocheza katika mashindano yote ya klabu na taifa.

Umri wake

Haki miliki ya picha
Getty Images

Unapotazama takwimu zake bila kutazama kitu chengine chochote unaweza kumlinganisha mchezaji huyo na wachezaji wengine ambao ni wakongwe katika soka.

Mchezaji huyo tayari ameshinda mara tatu mfululizo taji la ligi ya Uingereza. Alishinda kombe la ligi nchini humo katika msimu wake wa tatu wakati alipoelekea PSG.

Kylian ametambuliwa kama mchezaji mchanga wa mwaka katika ligi hiyo mbali na kushinda taji la mchezaji bora

Aliwahi kushinda zawadi ya ufungaji wa magoli mengi katika ligi hiyo ya Ufaransa mbali na kushinda taji la Kombe la dunia akiwa na umri wa miaka 19

Akishiriki katika michuano hiyo Mbappe alifunga goli katika fainali dhidi ya Croatia na kuwa kijana wa kwanza kufanya hivyo tangu Pele katika kombe la dunia la 1958.

Tofauti iliopo kati ya Mbappe na mkongwe huyo wa soka nchini Brazil Edson Arantes do Nascimento alishinda kombe la dunia akiwa na umri wa miaka 17 pekee.

Je ni wachezaji gani wanaolinganishwa na Mbappe?

Unapozungumzia kuhusu rekodi ya Mbappe utalazimika kuingia katika historia ya kandanda ambapo ni wachezaji watatu pekee waliofikia idadi hiyo ya magoli katika soka ya kulipwa.

Wachezaji nyota wa sasa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo hawahusiki kamwe kwa kuwa wote wawili walitinga magoli 100 kila mmoja wao walipokua na umri wa miaka 22.

Mchezaji wa kwanza aliyefikisha idadi hiyo kabla ya kufikia umri wa miaka 21 ni mkongwe wa Uingereza Jimmy Greaves.

Mchezaji huyo wa timu ya Engaland alifikisha idadi ya magoli hayo katika mmiaka yake minne ya kwanza akiichezea Chelsea na baadaye akahamia katika klabu ya Tottenham.

Mchezaji wa pili ni Ronaldo Nazario ambaye alifunga goli lake la 100 katika mwaka wake wa kwanza akiichezea klabu ya PSV Eindhoven.

Na mchezaji maarufu aliyevunja rekodi alikuwa Pele wa Brazil ambaye alikaribia kufunga goli lake la 200 kabala ya kuwa na umri wa miaka 21.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *