Mbio za Formula One kuanza kutimua vumbi


Msimu huu ambao awali ulilenga kuwa na mbio 22, umekwama tangu mbio za ufunguzi za Asutralian Grand Prix mnamo Machi 15 zilipofutwa kutokana na janga la COVID-19.

Mbio za kwanza mwaka huu zitakuwa Austria Jumapili Julai 5 na itakuwa mara ya kwanza kwa nchi moja kuandaa mikondo miwili ya Grand Prix katika mwaka mmoja. Muingereza Lewis Hamilton wa timu ya MERCEDES analenga kuwinda taji lake la saba la dunia “Nitaendelea tu kupambana na kujaribu kushinda zaidi, sio rahisi na kila mwaka inakuwa vigumu sana kwetu kwa sababu ushindani unakuwa mzuri na mgumu zaidi, na bila shaka bado tupo katika kipindi cha masharti yale yale kwa hiyo wengine wana nafasi ya kujaribu kutufikia. kwa hivyo nadhani utaona kinyang’anyiro kikali zaidi kuwahi kushuhUdiwa.” Amesema Hamilton

Baada ya mbio za Austria, magari hayo yataelekea Uingereza mnamo Agosti 5.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *