Meli iliyokataliwa kufuatia hofu ya COVID-19 yakubaliwa Cambodia


Mamia ya abiria walishangilia walipowasili na kushuka katika meli hiyo nchini Cambodia, ambapo walikaribishwa na kiongozi wa nchi hiyo, Hun Sen, aliyewapa maua. Waziri mkuu huyo aliamua kuiruhusu meli hiyo ya Westerdam kutia nanga katika bandari ya Sihanoukville hapo jana baada ya Thailand , Japan, Taiwan, Ufilipino na Guam kukataa kuiruhusu katika nchi hizo.

Wakati abiria wa kwanza aliposhuka kutoka meli hiyo, Hun Sen alisema kuwa ijapokuwa Cambodia ni nchi maskini, wakati wote imeungana na jamii ya kimataifa kutatua matatizo yanayoikumba dunia na eneo lao.

Meli hiyo ya Westerdam ilizuiliwa kutia nanga kwengineko ijapokuwa kampuni inayoimiliki ya Holland America Line inasema hakuna visa vya ugonjwa wa COVID-19 vilivyothibitishwa miongoni mwa abiria wake 1,455 na wafanyikazi 802.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *