Meli ya 'kijasusi' ya Iran yashambuliwa kwa makombora Bahari ya Shamu


Photograph released by the Saudi-led coalition in Yemen in 2018 purportedly showing speedboats on the deck of the Saviz

Chanzo cha picha, CIC

Maelezo ya picha,

Saudia na washirika wake katika vita nchini Yemen wanadai Saviz ni meli ya kijeshi ya Iran

Meli ya mizigo ya Iran imeshambuliwa kwa mlipuko ikiwa imetia nanga katika pwani ya Bahari ya Shamu nchini Yemen. Meli hiyo inadaiwa kutumiwa na kitengo maalum cha jeshi la Iran kwa kazi za kijasusi.

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imethibitisha shambulia hilo.

Mlipuko huo uliolenga meli hiyo kwa jina Saviz Jumanne haukusababisha majeruhi yoyote na shambulio hilo linafanyiwa uchunguzi, msemaji wa wizara hiyo amesema.

“Ilikuwa ni meli ya kiraia iliyowekwa hapo kulinda eneo hilo dhidi ya maharamia,” aliongeza.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *