Mfalme wa Ubelgiji asikitishwa na unyanyasaji wa wakati wa ukoloni Congo


King Philippe of Belgium, left, and President Félix Tshisekedi of DR Congo

Maelezo ya picha,

Mfalme Philippe ameonyesha kusikitishwa na unyanyasaji wakati a ukoloni katika barua aliyomuandikia rais Félix Tshisekedi wa Congo

Mfalme wa Ubelgiji Philippe ameonesha masikitiko yake juu ya unyanyasaji wa kikoloni wa nchi yake uliofanyiwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mfalme anayetawala amesema hayo katika barua aliyotuma kwa rais Felix Tshisekedi wakati nchi hiyo inaadhimisha miaka 60 tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji.

Ubelgiji ilitawala nchi hiyo ya katika mwa Afrika kuanzia karne ya 19 hadi ilipojinyakuliwa uhuru wake 1960.

Mamilioni ya Waafrika walikufa wakati wa utawala wa ukoloni ulioghubikwa na umwagikaji damu

Kuna angalizo jipya la historia ya mataifa ya Ulaya baada ya kifo cha George Floyd aliyekufa mikononi mwa polisi huko Marekani na maandamano ya Black Lives Matter yakafuata kote nchini humo.

Maelfu ya raia wa Ubelgiji wameandamana katika wiki za hivi karibuni na masanamu ya aliyekuwa mfalme wakati wa ukoloni Ubelgiji, Leopold II, yameharibiwa.

Mamlaka huko Antwerp imeondoa sanamu la kiongozi huyo kutoka eneo la umma.

Zaidi ya raia wa Afrika milioni 10 inaaminika kwamba walikufa wakati wa utawala wake. Mfalme Philippe ni uzao wa moja kwa moja wa mtawala wa karne ya 19.

Mfalme Philippe amesema nini?

Hii ni mara ya kwanza mfalme anayetawala ameonesha kusikitishwa na kilichotokea wakati wa utawala wa kikoloni chini ya nchi yake.

Katika barua aliyoiandika kwa rais Tshisekedi na kuchapishwa katika vyombo vya habari vya Ubelgiji, mfalme Philippe alipongeza uhusiano wa nchi hizo mbili uliopo kwa sasa.

Lakini alisema kwamba kumekuwa na matukio ya kuumiza moyo katika historia ya nchi hizo ikiwemo wakati wa utawala wa Mfalme Leopold II – ambaye hakumtaja kwa jina moja kwa moja na pia karne ya 20.

Maelezo ya picha,

Wiki za hivi karibuni, raia wa Ubelgiji wameharibu masanamu ya Mfalme Leopold II

“Ningependa kuonyesha masikitiko yangu kwa kwa madhila yaliyotokea siku za nyuma, machungu ambayo sasa hivi yanaibuliwa tena kwasababu ya unyanyapaa ambao bado unaendelea katika jamii zetu,” King Philippe aliandika.

“Nitaendelea kupiga vita aina zote za ubaguzi wa rangi. Nahimiza mabadiliko ambayo yameanzishwa na bunge letu ili kumbukumbu zetu zimeze kutulia na kusonga mbele.”

Kama ilivyo kwa Uingereza, Ubelgiji ni nchi ya utawala na kumaanisha kwamba taarifa ya mfalme Philippe ilikubaliwa pia na serikali ya Waziri Mkuu Sophie Wilmès.

Mapema mwezi huu kaka ya mfalme Philippe, Mwana mfalme Laurent, alimtetea mfalme Leopold II.

“hakuwahi kwenda Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yeye mwenyewe,” mwanamfalme huyo alisema kwenye mahojiano. “Sioni ni kwa namna gani alisababisha watu kutaabika.”

Mtazamo wa Wakongo kuhusu uhuru ni upi?

Kulingana na wakaazi mwaka huu hakuna kusherehekea kulingana na matatizo mengi ya kiafya hasa magonjwa.

Licha ya uhuru huu, raia wengi nchini Congo wanaendelea kuishi katika hali mbovu.

Ajabu ni kwamba kuna wanaopendelea nyakati za ukoloni zaidi kuliko hali ilivyo kwa sasa.

Mwandishi BBC, Kinshasa, Mbelechi msoshi amezungumza na Bi Asha Egeuni ambaye alishuhudia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikipata uhuru wake miaka sitini iliyopita.

“Tuliona uhuru wetu bado tukiwa watoto wadogo, tuliona wazungu wanakuja vijijini, wakija tu na gari za jeshi, wazazi wetu walikuwa wana wakimbilia moja kwa moja”

Bi. Asha anakumbuka wakati wa ukoloni chini ya ubelgiji anasema hakujua kama mtu analipa pesa ili apate matibabu hosptalini na pia chakula kolikuwa rahisi sana.

Bibi huyu ambae leo ana miaka sitini na minane, amesema anahisi kuwa wanasisia wakongo hawakuwa tayari kuongoza nchi yenyewe.

“Tulikuwa tunapewa matibabu ya bure, ukinunua chakula ya pesa za Congo elfu tatu, utapika chungu kizima cha nyama lakini kwa sasa, hizo pesa hazitoshi tena, unapata tu mnofu kidogo kisha watoto wanakula ugali na supu”

Lakini pengine kipi kilichangia Jamhuri ya Kidemokrasia ya ongo kurejea tena nyuma baada ya kupata uhuru?

Profesa …Jean Pierre Bayolo ni mwanahistoria

“Rais Mobutu alifanya eti mali yote ya Congo iwe mikononi mwa wanakongomani wakati bado hawajakuwa na ujuzi kuhusu uongozi bora.

Alifanya hata mradi wake ambao uliitwa zairani zation yaani kufanya kitu chote kiwe chini ya uongozi wa mkongomani, alikataa wageni kuongoza.

Wakati huu ndio mambo yote yaliharibika kwasababu namna wa wakongo walivyoongoza haikuruhusu kulinda vizuri uchumi wa nchi”

Aidha serikali mwaka huu iliamua kutosherehekea maadhimisho ya miaka sitini ya uhuru wa Congo kulingana na jinsi nchi inakabiliwa na milipuko kadhaa, yaani Ebola, Covid-19 , ugonjwa wa surua na kadhalika.

Kwa mujibu wa serkali, pesa zote zinazopaswa kusherehekea siku ya uhuru zitatengwa na kusaidia kupambana dhidi ya magonjwa hayo.

Historia inasema nini?

Karne ya 19, nchi za Ulaya zenye nguvu zilianza kuingia Afrika ili kuzitawala.

Mfalme Leopold II alikabidhiwa udhibiti w eneo kubwa kuzunguka bonde la mto Congo – ambalo kwa sasa inafahika kama Nchi Huru ya Congo

Kati ya mwaka 1885 hadi 1908 raia wa Afrika zaidi ya milioni 10 inaanimika kwamba walikufa kwasababu ya magonjwa na dhulma za ukoloni wakati wanafanyakazi katika mashamba ya mfalme.

Hali ilikuwa mbaya zaidi huku nchi zingine zikiweka wazi kilichokuwa kinaendelea na kushtumu madhila yaliyotekelezwa.

Mfalme Leopold II aliacha kudhibiti Congo moja kwa moja 1908, na Ubelgiji ikatwaa rasmi eneo hilo na kulipa jina la Belgian Congo.

Wakoloni waliendelea kutumia raia wa Afrika kama wafanyakazi. Lakini kwasababu ya upinzani kutoka kila pembe hatimaye nchi hiyo ilijinyakulia uhuru wake 1960.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *