Mke wa El Chapo Emma Coronel Aispuro akamatwa Marekani kwa 'Ulanguzi wa mihadarati'


Emma Coronel Aispuro alisalia mtiifu kwa mume wake kila siku katika kesi yake ya 2019

Maelezo ya picha,

Emma Coronel Aispuro alisalia mtiifu kwa mume wake kila siku katika kesi yake ya 2019

Mke wa mlanguzi mkuu wa mihadarati kutoka Mexico El Chapo Guzman amekamatwa nchini Marekani kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati , imesema mamlaka nchini humo.

Emma Coronel Aispuro , mwenye umri wa miaka 31 alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles nje ya mji mkuu wa Washington DC.

Anashtakiwa kwa kushiriki katika njama ya kutaka kusambaza dawa aina ya Cocaine, Methamphetamine, heroin na bangi.

Guzman kwasasa anahudumia kifungo cha maisha jela mjini New York kwa kuhusika katika ulanguzi wa mihadarati na fedha.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *