Mo Dewji bado ni mmoja wa mabilionea 20 kutoka Afrika – ForbesKutoka Afrika Mashariki, Mohammed Dewji, mfanyabiashara tajika na raia wa Tanzania ametajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 20 wa bara hilo, akishikila nafasi ya 16.

Hata hivyo, utajiri wa bilionea huyo, ambaye anamiliki klabu cha kandada cha Simba, umedaiwa kupungua hadi dola bilioni 1.6.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya, Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara za aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uzalishaji na uuzaji wa saruji, Sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1.

Dangote anafuatiwa na mfanyabiashara wa Misri Nassef Sawaris, ambaye aliongeza utajiri wake kutoka dola bilioni 6.3, alizokuwa nazo mwaka uliopita, hadi dola bilioni nane.

Isabel dos Santos mwenye utajiri wa dola bilioni 2.2, ameendelea kushikilia taji la mwanamke tajiri Zaidi barani Afrika.

Inaaminika kwamba Bi Dos Santos alijipatia utajiri wake wakati babake alipokuwa rais ambapo alianza kumiliki hisa katika makampuni mengi ya Angola pamoja na benki.

wa aliyekuwa rais wa Angola Isabel dos Santos ni miongoni

Wakati huo huo, Katika orodha ya watu wanne matajiri zaidi duniani, Bernard Arnault, sasa ndiye mtu tajiri zaidi duniani akiwa na mali yenye thamani ya dola billioni 116.5.

Bernard anamiliki kamapuni ya mitindo ya Louis Vuitton na Sephora.

Jeff Bezos, kutoka Marekani, anayemiliki mali yenye thamani ya dola bilioni 115.6 alitangazwa kuwa mtu wa pili kwa utajiri zaidi duniani, huku nafasi ya tatu ikienda kwa mjasiriamali tajika, Bill Gates, mwenye mali yenye thamani dola bilioni 110.6.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *