Mwanamfalme Andrew atatakiwa kutoa ushahidi anasema wakili wa mlalamikaji Epstein


Wanawake watano wanaomshutumu Jeffrey Epstein kuwanyanyasa anasema Mwanamfalme Andrew alishuhudia jinsi watu walivyokua wakisingwa katika nyumba za mtu anayeshutumiwa kutekeleza uhalifu wa kingono.

Wakili wa wanawake hao ameiambia BBC Panorama kwamba anapanga kuwasilisha mapendekezo kwa mahakama yatakayomshinikiza the Duke of York kutoa ushahidi katika kesi zote tano.

Anasema mwanamfalme anaweza kuwa na taarifa muhimu kuhusu biashara ya ngono.

Mwanamfalme anasema hakushuhudia au kushuku mwenendo wowote usiofaa wakati alipozitembelea nyumba za Epstein.

Epstein alijiua katika mahabusu ya gereza mwezi Agosti akiwa na umri wa miaka 66, alipokua akisubiri kesi juu ya mashitaka ya biashara ya ngono dhidi yake.

Wakili wa waathiria wa Marekani , David Boies alisema: “Moja ya mambo ambayo tumeyajaribu ni kumhoji Mwanamfalme Andrew na kujaribu kupata maelezo yake ni. Amekua akizuru mara kwa mara nyumba hizo. Wanapaswa kuwasilisha mahojiano. Wanapaswa kuzungumzia juu yake .”

Maagizo ya mahakama yanayomuita kutoa ushahidi yameandaliwa kwa ajili ya kesi zote tano na zitatakiwa kusainiwa na jaji wakati Mwanamfalme atakapoingia katika ardhi ya Marekani.

Baada ya hapo atakuwa na uwezo wa kupinga agizo la mahakama mahakamani kama hatotaka kutoa ushahidi.

Image caption

Virginia Giuffre

Kipindi cha uchunguzi cha BBC Panorama pia kilifichua kuwa taarifa mpya juu ya picha ya Mwanamfalme Andrew yenye utata ambapo alionekana mkono wake ukiwa umemzunguka mshichana mwenye umri wa miaka 17 Virginia Giuffre – wakati huo akiitwa Virginia Roberts.

Msichana huyo alisema kuwa yeye, mwanamfalme, Epstein na aliyekuwa rafiki yake wa kike, aliyekuwa maarufu sana katika mitandao ya kijamii Ghislaine Maxwell, walikwenda katika ukumbi wa starehe wa usiku unaofahamika ma Tramp mjini London.

Bi Giuffre alisema kwamba katika gari walipokuwa wakirfudi kutoka katika ukumbi huo “Ghislaine aliniambia kuwa ninapaswa kumfanyia Andrew kile ninachomfanyia Jeffrey na hilo liliudhi sana”.

Waliporudi nyu,mbani, alisema alimuuliza Epstein ampige picha ambayo angeionyesha familia. Halafu akatekeleza miongozo aliyopewa ya kumburudisha mwanamfalme Andrew.

“Kulikuwa na bafuna mambo yalianzia pale na yakaendelea hadi katika chumba cha kulala na haikuchukua muda mrefu sana, utaratibu mzima .

“Ilikuwa inaudhi, si kwamba hakua mkaribu au lolote, lakini aliamka na akasema asante na akaondoka nje.”

Ni picha halisi

Mwnamfalme Andrew anakana kufanya ngono ya aina yoyote au kuwa na uhusiano na Virginia Giuffre na anasema dai lolote kinyume na ni uongo usio na msingi wowote.

Alisema kuwa hakumbuki kabisa kuwa alikutana na Virginia Giuffre.

Haki miliki ya picha
Virginia Roberts

Image caption

Virginia Giuffre anaelezea jinsi alivyomuomba Jeffrey Epstein kumpiga picha yake na Andrew

Picha yao pamoja ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2011 baada ya gazeti la Mail Jumapili kumpata Bi Giuffre na kumlipa $160,000 ili asimulie hadithi yake.

Mwaka huu duru za ufalme wa uingereza zilianza kusema picha ilikuwa ni feki- lakini Mwanamfalme Andrew alisitisha madai hayo katika mahojiano yake na kipindi cha BBC Newsnight.

Alisema : ” Hauwezi kuthibitisha kama picha ni feki au sio feki kasababu ni picha ya picha ya picha .”

“Ni vigumu kuweza kuithibitisha lakini sikumbuki picha hiyo ikipigwa. Huyo ni mimi lakini kusema huo ni mkono wangu …hakika sikumbuki picha ikipigwa.”

Mwanamfalme pia alisema kuwa anafikiri hajawahi kwenda kwenye sehemu ya juu ya nyumba ya rafiki yake Ghislaine Maxwell, ambako picha hiyo inaonekana ilichukuliwa.

Lakini Bi Giuffre alikiambia kipindi cha Panorama picha hiyo ilikuwa ni nakili ya picha halisi na alilipatia shirika la ujasusi la Marekani picha yenyewe mnamo mwaka 2011.

” Ninadhani dunia imechoshwa na sababu hizi za kijinga. Ni picha halisi,” alisema. ” Nimekwisha itoa kwa FBI kwa ajili ya uchunguzi na ni picha ya kuaminika. Ina tarehe ya siku iliyochukuliwa nyuma yake”

Alisema tarehe iliyopo nyuma ya picha ni 13 Machi 2001 -siku mbili baada ya kuondoka kutoka London kwa matembezi na Epstein na Bi Maxwell.

Panoramapia ilizungumza na wapigapicha wa kibinafsi Michael Thomas ambaye alitoa nakala ya kwanza mwaka 2011.

Anaamini kuwa picha hiyo ni halisi kwasababu aliipata katikati ya lundo la picha ambazo Bi Giuffre alimkabidhi ali[potoka katika matembezi yake na Epstein na Bi Maxwell.

Unaweza pia kusoma:

Alisema : “Hakuna kitu kigumu : Zilikua ni picha zaukubwa wa 5×7 ambazo zilionekna kana kwamba zilitoka katika madukaya dawa ya Boots. Zilikuwa ni picha za kawaida za msichana mdogo.”

Kipindi hicho cha BBC pia kilibaini ushahidi unaoonyesha kwamba madai ya Bi Giuffre kwamba alitoa nakala halisi kwa FBI yalikuwa ni ya kweli.

Nyaraka za mahakama zinaonyesha kuwa alitoa picha 20 kwa FBI mwaka 2011 na zikafanyiwa skani mbele na nyuma.

Lakini kuna 19 pekee zilizoonyeshwa kwa umma.

Panorama imeambiwa kuwa picha ya Mwanamfalme Andrewiliondolewa kwa umma ili kulinda taarifa zake za kibinafsi.

Muathiriwa mwingin wa vitendo vya Epstein, Sarah Ransome alikiambia kipindi cha Panorama kuwa Ghislaine Maxwell, mmoja wa marafiki wa zamani sana wa mwnamfalme Andrew alifanya kazi bega kwa bega na Epstein.

“Ghislaine aliwadhibiti wasichana . Alikuwa nikama Madam,” alisema.

“Alikuwa ni kama mkuu wa shughuli za biashara ya ngono na kila mara alimtembelea Jeffreykatika kisiwa ili kuhakikisha wasichana wanafanya kile ambacho walipaswa kukifanya.

“Alifahamu fika ni nini Jeffrey anapenda. Alifanya kazi na kusaidia kuimarisha viwango vya Jeffrey kwa kuwatisha wasichana, kwa hivyo hizi zilikuwa ni juhudi za pamoja.”

Bi Maxwel hakuweza kupatikana kutoa maoni yake , lakini awali alikana kuhusika kwa namna yoyote ile au hata kufahamu lolote juu ya unyanyasaji wa Epstein.

Madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi yake yalitangazwa kwa umma katika nyaraka za mahakama mnamo mwaka 2009, lakini Mwanamfalme Andrew ameendeleza urafiki.

Haki miliki ya picha
Tim Graham

Image caption

mwanamfalme Andrew na Ghislaine Maxwell walihudhuria sherehe mwezi June 2000.

Kipindi cha Panorama kiligundua ujumbe wa baruapepe wa mwaka 2015 unaoonyesha kuwa hata alimuomba Bi Maxwell msaada katika kushughulikia madai ya Virginia Giuffre. Alifahamika wakati huo kwa jina bandia la Virginia Roberts.

Katika baruapepe hiyo mwanamfalme alimuambia Bi Maxwell: ” Nifahamishe ni lini tunaweza kuongea. Nina maswali ya kipekee ya kukuuliza kumuhusu Virginia Roberts.”

Alijibu: “Nina taarifa. Nipigie simu utakapokuwa na muda.”

Mwanamfalme Andrew alikataa kujibu maswali yenye maelezo ya kipindi cha Panoramalakini akasema katika taarifa kwamba haungi mkono unyasaji wowote dhidi ya binadamu na hawezi kuhusika au kuunga mkono tabia yoyote ya aina hiyo.

“Mwanamfalme Andrew anajutia kwa namna anavyochukuliwa vibaya na umma juu ya uhusiano Jeffrey Epstein. Kujiua kwa Epstein kuliacha maswali mengi bila majibu, hususan kwa waathiriwa wa unyanyasaji wake. Mwanamfalme anasema anasikitishwa sana na wale walioathiriwa ambao wanataka aina fulani ya haki.

“Nimatumaini yake kwamba, baada ya muda wataweza kujenga upya maisha yao. Mwanamfalme yuko tayari kutoa usaidizi wowote kwa maafisa wa usalama katika uchunguzi, ikiwa atahitajika kufanya hivyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *