Mwanamfalme wa Saudi ashutumiwa kwa kutuma mamluki Canada


Saad al-Jabri (circled) accompanies Prince Mohammed bin Nayef (centre) during a visit to London in 2015, with

Maelezo ya picha,

Saad al-Jabri (aliyezungushiwa alama ya mduara) akikaribishwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Theresa May (kulia) alipotembelea London 2015

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa wa ujasusi wa Saudi.

Mpango huo wa kumuua Saad al-Jabri ambao haukufanikiwa ulifuata muda mfupi baada ya mauaji ya mwanahabari aliyeuawa nchini Uturuki, Jamal Khashoggi, nyaraka zilizoawasilishwa katika mahamakama ya Marekani zimedai. .

Bwana Jabri, afisa mstaafu wa serikali ya Saudi Arabia, alikimbilia ughaibuni miaka mitatu iliyopita.

Tangu wakati huo amekuwa akipewa ulinzi binafsi mjini Toronto.

Mpango huo wa mauaji inasemekana kuwa ulifeli baada ya maafisa wa mpaka wa Canada kuanza kushuku kikosi hicho walipokuwa wanajaribu kuingia nchini humo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Toronto Pearson, nyaraka zilizowasilishwa mahakamani zinaonesha.

Kwa miaka mingi, Bwana Jabri, 61, alikuwa kiungo muhimu katika huduma ya ujasusi ya siri Uingereza na mashirika mengine ya kijasusi ya nchi za Magharibi nchini Saudi Arabia.

Mashtaka yanasema nini?

Malalamiko ya kurasa 106 ambayo bado hayajaidhinishwa, yalifunguliwa Washington DC, yakimshutumu mwanamfalme kwa kujaribu kumuua Bwana Jabri ili kumyamazisha.

Bwana Jabri anasema hilo ni kwasababu yeye anajua taarifa nyeti. Nyaraka inasema hayo ni pamoja na ufisadi na usimamizi wa kikundi cha mamluki nje ya nchi kilichopewa jina la kikosi cha Tiger.

Wanachama wa kikosi cha mamluki cha Tiger walihusika na mauaji ya mwanahabari Khashoggi, aliyeuliwa ndani ya ubalozi wa Saudi, mjini Istanbul 2018, nyaraka iliyowasilishwa mahakamani inasema.

“Sehemu ya madai ni nyeti, ikiwa ni pamoja na tarifa za udhalilishaji na nyingine zenye ushahidi kuhusu mshtakiwa bin Salman na kumbukumbu ya Dkt. Saad inavyoangazia nukuu alizosema akibashiri kuuawa kwakwe,” nyaraka hiyo inasema.

“Hiyo ndio sababu mshitakiwa bin Salman anataka auawe, na pia ndio sababu bin Salman amekuwa akifanyia kazi lengo hilo kuhakikisha linafanikiwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.”

Baada ya kutoroka Saudi Arabia 2017, Bwana Jabri alikimbilia Canada kupitia Uturuki.

Anadai kwamba Bwana Mohammed bin Salman alifanya majaribio kadhaa ya kumrejesha Saudi Arabia, kiasi cha hata kutuma ujumbe wa kibinafsi, ikiwemo ule uliosema: “Bila shaka hatimae tutakukamata tu”.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *