Mwanamke aliyang’ang’ania mayai yake ya ziada ya uzazi


Ashley's three children
Maelezo ya picha,

Watoto watatu wa Ashley

Ashley Strong ana watoto watatu aliowapata kupitia uzazi wa usaidizi wa maabara kwa lugha ya kitaalamu IVF.

Anafahamu fika kwamba hahitaji kupata watoto zaidi, lakini kila mwaka analipia gharama za kuyatunza kwenye friji mayai yake matatu ya uzazi ili yaendelee kutunzwa katika kliniki ya uzazi IVF.

IVF ni uzazi unaohusisha kuungana kwa yai la mwanamke na mbegu za kiume kwenye maabara.

“Ninaendelea kulipa kwasababu sijafanya uamuzi, ” alikiambia kipindi cha 5 Live cha Emma Barnett nchini Uingereza.

Kila mwaka kliniki hiyo humuandikia barua kumuuliza ni nini anachotaka kuyafanyia mayai yake, lakini bado hajaweza kukubali kuachana nayo.

“Barua inakuja kila mwaka,” Ashley anasema.

“Ninang’angana nisiifungue au kuiangalia kwa muda mrefu kujaribu kujipatia muda kufikiria kuhusu mayai yangu.

“Mayai yangu ya uzazi yametunzwa kwa miaka minane sasa na bado hata sijakaribia kuchukua uamuzi kuyahusu .”

Baadhi ya watu wanapata matibabu ya kusaidiwa kutungishwa mimba wanakuwa na mayai yaliyobaki baada ya kufanyiwa IVF.

Badala ya kuyatupa unaweza kuyatunza katika friji kwa ajili ya matumizi ya siku za usoni iwapo jaribio la kwanza la kurutubishwa kwa mayai yako ya uzazi halijafanikiwa au ukihitaji tena kupata mtoto au hata kumpatia ndugu yako anayehitaji mtoto.

Chini ya mwongozo maalum, watu wanaweza kuyatunza mayai yao ya uzazi kwa hadi miaka 10. Baada ya muda huo, wanatakiwa kuamua ni nini wanachotaka kuyafanyia- ama kuyatumia wenyewe, kuyatoa kama msaada au, kama teknolojia inavyoeleza, “kuyaacha yaishie”.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya usaidizi wa uzazi kwa wa binadamu na kiini (HFEA), utunzaji wake unagarimu pauni kati ya 125 na 350 kwa mwaka.

“Kufahami kwamba ukomo wa miaka 10 unafikia ukingoni na mtu anatakiwa kuchukua uamuzi kwa ajili yangu lilikuwa ni jambo nililolisubiri ,” anasema Ashley sa

“Lakini nilipata barua wiki kadhaa zilizopita ikisema, kwasababu ya Covid, wataongeza muda miaka miwili zaidi. Nilifikiria hiyo inamaanisha kuwa nitalipia mayai yangu kwa miaka miwili tena zaidi ‘.

” Kusema ukweli, nilifikiri nitachukua uamuzi wa hatma ya mayai yangu , lakini ni vigumu sana kuwa ninaweza kuchukua uamuzi bila kupata ushauri nasaha.

Maelezo ya picha,

Ashley ameunganishwa kihisia na mayai yake jambo linalomfanya kuhisi ugumu wa kufanya maamuzi kuyahusu

Sehemu moja ya ugumu wa kuchukua maamuzi ni kwamba mayai hayo yanamkumbusha matatizo aliyoyapitia katika kuwapata watoto.

“Tumepitia kipindi kigumu sana…Mimba nyingi zimetoka, masikitiko makubwa, kwa hiyo kukubali mayai yangu ya uzazi yapotee tu ni vigumu sana kwangu .”

Anasema mume wake hana hisia sana kuyahusu mayai yake sawa na ilivyo kwake na “angefurahia sana kama tungeyatoa kama msaada “. Lakinikwake kuna hisia zinazoambatana nayo ambazo zinamzuwia kuchukua maamuzi.

Maelezo ya picha,

Natalie Silverman alikutana na mshauri nasaha ili akubali mchakato kuhusu kuacha mayai yake ya uzazi

Natalie Silverman na mume wake wana mtoto mvulana mwenye umri wa miaka mitanoambaye walimpata kwa njia ya IVF. Walisaidiwa kulipia garama ya kutunza mayai kwa kipindi cha mwaka mmoja, lakini baadaye walitakiwa kulipia garama hizo wenyewe.

Taratibu walikuja kugundua kuwa hawana uwezo wa kumpata mtoto mwingine, au kuendelea kulipia garama ya mayai yaliyohifadhiwa.

Natalie ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha podcast kuhusu uzazi, alipata ushauri nasaha katika kipindi cha miezi 18 ili kumsaidia kuukubali mchakato wa kuachana na mayai yake.

Kwangu mimi ni uamuzi mgumu sana kwasababu unachukua uamuazi wa kutoweza kufanya kitu fulani daima. Unasema : ‘Inamaanisha unasema sitakuwa tena na watoto zaidi ,'” anasema.

Kusema kwaheri

Kuamua cha kufanyia viini tete vyao ulikuwa ni uamuzi mkubwa pia. Natali alisema kuwa kuvitoa kama msaada kwa watu waliooana halikuwa chaguo lake kwasababu asingependa kufikiria kuwa kuna ” mtu mwingine anayefanana na mtoto wangu wa kiume “.

Badala yake, Natalie na mumewe waliamua kutoa msaada wa viini tete hivyo kwa wanasayansi na akasema shukrani walizopokea kutoka kwa wanasayansi hao ziliwafanya wafurahie uamuzi wao.

“Wataalamu wa uzazi wa kusaidiwa na viini tete wanaona wanaona msaada wako kama kitu cha thamani. Wanaelezea msaada wa viini tete kama zawadi na wanazungumzia kuhusu viini tete kama kitu cha thamani ,” anasema.

“Ilinifanya kwa kiasi kikubwa kuhisi kuwa hiki ndicho kitu ambacho kinaweza kunisaidia kutua mzigo niliyoubeba kichwani wa kuyafikiria mayaio yangu ya uzazi .”

Natalie na mume wake walitoa msaada wa viini tete vyao mwezi Februari -mchakato mrefu uliohusisha kusainiwa kwa makaratasi mengi. Lakini baada ya hapo walifanya sherehe ya kusema kwaheri kwa watoto wao ambao hawaweza kuwaona tena.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *