Mwenye uraia wa Uingereza na Iran akamatwa Iran


Mke wa Kameel Ahmady (kulia ) amesema hajafahamishwa juu ya mashtaka dhidi yake

Haki miliki ya picha
FACEBOOK

Image caption

Mke wa Kameel Ahmady (kulia ) amesema hajafahamishwa juu ya mashtaka dhidi yake

Mtu mwenye uraia wa nchi mbili Uingereza na Iran amekamatwa magharibi mwa Iran, kwa mujibu wa familia yake.

Mkewe Kameel Ahmady, ambaye ni mtaalamu wa historia ya binadamu na jamii , amema kuwa alipelekwa mahabusu Jumapili kutoka nyumbani kwake bila kuelezwa sababu.

Bwana Ahmady amefanya utafiti kuhusu ukeketaji wa wanawake pamoja na ndoa za watoto nchini Iran , miongoni mwa tafiti zingine.

Muingereza mwingine mwenye uraia wa wa nchi hizo mbili , Nazanin Zaghari-Ratcliffe, amekuwa katika mahabusu ya Iran tangu mwaka 2016 juu ya madai ya kufanya ujasusi.

Mapema mwaka huu , wizara ya mambo ya nchi za nje ya Uingereza iliwashauri watu wote wenye uraia wa nchi mbili wasisafiri kwenda Iran kwasababu wako katika hatari ya kukamatwa bila kiholela.

Kukamatwa kwa hivi karibuni kwa Ahmady kunatokea huku kukiwa na hali ya wasiwasi baina ya nchi hizo , kutokana na kukamatwa kwa meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya Uingereza.

Wavuti wa wasoni ulilitaja jina la Ahmady ukimuelezea kama “Muingereza-Muiran asilia kutoka Kurdistan”. Utambulisha wake wa wavuti Kitaaluma LinkedIn unasema alisomea katika vyuo vikuu vya Uingereza kikiwemo -London School of Economics na Political Science (LSE).

Haki miliki ya picha
Facebook

Image caption

Kameel Ahmady aliandika vitabu na makala kadhaa

Msemaji wa Mtandao wa Haki za kinadamu wa Kurdistan , ulioripoti kukamatwa kwake , umesema kuwa Bwana Ahmady ameishi Iran kwa miaka mingi.

Maafisa katika nchi zote mbili bado hawajathibitisha kuwa amepelekwa mahabusu.

Katika mahojiano na Idhaa ya BBC ya Kipershi BBC , mkewe Shafaq Rahmani alidai kuwa maafisa wa usalama walikuja kwenye nyumba yao na ” kuchukua stakabadhi, ikiwemo kadi ya kitambulisho “.

Amesema , afisa mmoja wa mahakama katika eneo hilo baadae alithibitisha agizo la kifungo cha muda cha mwezi mmoja limetolewa dhidi ya Bwana Ahmady.

“Hawajatoa taarifa yoyote juu ya sababu ya kumkamata au hata mashtaka dhidi ya Kameel,” Bi Rahmani aliandika katika Instagram.

Iran haitambui utaia wa nchi mbili na hakuna yakwimu kamili juu ya idadi ya watu waliokamatwa ambao pia wana uraia wa nchi za kigeni.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *