Mzozo kati ya Misri na Ethiopia: Nani anayemiliki wa mto Nile


Bwawa la Grand Renaissance ni chanzo cha fahari ya kitaifa kwa Ethiopia

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Bwawa la Grand Renaissance ni chanzo cha fahari ya kitaifa kwa Ethiopia

Mazungumzo ya hivi karibuni ya kutatua mgogoro kati ya Ethiopia na Misri kuhusu hatma ya mradi wa bwawa kubwa la uzalishaji umeme katika mto Nile, yanatarajiwa kurudiwa nchini Marekani.

Mwaka jana waliweka siku ya mwisho ya kupata suluhu ya mgogoro huo kuwa Januari 15, lakini mpaka sasa hakuna kilichotatuliwa kwa sababu hata mazungumzo yaliyofanywa wiki iliyopita bado hayakuwa na uelekeo wowote.

Ujenzi huo wa bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia utakuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme barani Afrika.

Ujenzi huo ulianza mwaka 2011 kaskazini mwa Ethiopia ambapo maji yatakayotumika ni 85% ya maji yanayotiririka kutoka mto Nile.

Hata hivyo ujenzi huo umesababisha kuwepo kwa mzozo kati ya Misri na Ethiopia, huku Sudan pia ikihusishwa na sasa Marekani inajaribu kutatua mzozo huo.

Kwa nini kuna mvutanokuhusu ujenzi huo?

Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji na kuifanya Ethiopia kuwa na mamlaka juu ya usambaaji wa maji ya mto mkubwa Afrika.

Kituo cha kuzalisha umeme hakitatumia maji bali bwawa hilo linalojengwa na Ethiopia litaathiri kwa kiwango kikubwa kasi ya mtiririko wa maji.

Muda mrefu utakaotumika kuweka maji katika bwawa ambalo linaenda kuwa kubwa zaidi ya London, inaweza kuleta matokeo pungufu katika kiwango cha mto.

Ethiopia inataka kuweka mradi huo kwa miaka sita.

“Tuna mpango wa kuanza kujaza bwawa hilo katika msimu ujao wa mvua na tutaanza kuendesha mitambo miwili ya umeme kuanzia mwezi disemba mwaka 2020,” Waziri wa maji nchi Ethiopia, Seleshi Bekeli alisema mwezi septemba.

Licha ya kuwa Misri ilipendekeza kipindi cha miaka 10- hii ikiwa inamaanisha kuwa mto unaweza kuathirika sana katika mfumo wa usambazaji wa maji haswa kwenye hatua za awali.

Mazungumzo kati ya Misri, Sudan na Ethiopia ya namna ya kuendesha mradi huo wa bwawa na haujapiga hatua yoyote kwa miaka minne na sasa Marekani inajaribu kuwapatanisha.

Baada ya mazungumzo ya wiki iliyopita, bwana Seleshi imedai kuwa Misri haina nia ya kufikia makubaliano

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Waziri wa masuala ya maji nchini anasema kuwa wataanza kuweka maji katika bwawa, mwezi Julai

“Sidhani kama wawakilishi wa Misri walikuja ili kuafikiana katika jambo hili,” Bwana Seleshi aliiambia BBC.

“Kuna utaratibu mpya waliouandaa kupitisha maji katika bwawa hilo. Mfumo huo mpya utachukua miaka 12 mpaka 21 kujaza bwawa hilo.

“Hii haikubaliki kabisa kwa namna yoyote,” alisema.

Waziri wa maji nchini Misri, bwana Mohamed Abdel Aty, alinukuliwa kusema kuwa pande zote zinapaswa kukubaliana namna ya kujaza maji bwawa hilo.

Kwa nini Misri imekasirika?

Misri inategemea maji ya mto Nile kwa 85% .

Kihistoria, Misri inategemea kwa kiwango kikubwa cha maji ya mto Nile hivyo kama mfumo wa maji hayo utaathirika basi nchi nzima itaathirika.

Makubaliano ya mwaka 1929 iliwapa Misri na Sudan haki ya maji ya mto wote wa Nile.

Wakati wa ukoloni, Misri ilipewa kura ya turufu dhidi ya mradi wowote utakaoendeshwa katika maji hayo kuwa na mamlaka ya kuzuia kama utaathiri sehemu ya maji wanayoyapata.

Ethiopia inasema kuwa hakuna haja ya kuendelea kufungwa na makubaliano ya miongo mingi iliyopita na ndio maana ilianza ujenzi wa bwawa hilo mwaka 2011 bila ya kushauriana na Misri.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mto Nile unasambaza maji katika mji wa Aswan ambao ni maili 570 kutoka kusini mwa mji mkuu wa Cairo

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alinukuliwa mwezi septemba akisema kuwa ushawishi wa kisiasa hauwezi kuathiri mfumo wa mto huo.

Nchi za kaskazini mwa Afrika zinasema kuwa wasiwasi wao upo kwenye ziwa Nasser, ambalo linatengeneza umeme wa Misri.

Vilevile mradi huo wa usafirishaji unaweza kuathiri sekta ya usafirishaji kama kiwango cha maji kitashuka na kuathiri wakulima ambao wanategemea maji hayo katika kilimo cha umwagiliaji.

Kwa nini Ethiopia inataka kuwa na bwawa kubwa kiasi hicho?

Mradi huu mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme utakaogharimu dola bilioni nne unategemewa kuzalisha kiwango kikubwa cha umeme barani Afrika.

Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kutoa umeme wa nguvu ya ‘megawatts’ 6,000.

Ethiopia inakabiliwa na tatizo la uhaba wa umeme, zaidi ya 65% ya idadi ya watu nchini humo hawajaunganishiwa umeme.

Hivyo mradi huu ukifanikiwa, utawawezesha wananchi wake kupata umeme wa uhakika na kuuza mwingine kwa nchi za jirani.

Ethiopia inaona kuwa bwawa hilo ni suala linalohusu taifa husika.

Mradi wa bwawa hautegemei ufadhili kutoka nje bali inategemea maamuzi ya serikali na ufadhili binafsi ili kulipa mradi huo.

Taifa hilo limekosoa jinsi mataifa ya kigeni yanavyoingilia ujenzi huo.

Je, ujenzi huo una mnufaisha nani mwingine?

Sudan, Sudan kusini, Kenya, Djibouti na Eritrea ni mataifa ambayo yanatarajiwa kunufaika na mradi huo wa bwawa.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Ethiopia inategemea kumaliza ujenzi huo mwaka 2020

Mataifa mengi kati ya haya yana shida ya umeme.

Kwa upande wa Sudan, mradi huu utakuwa na manufaa zaidi kwa kipindi cha mwaka mzima kwa bwawa hilo kuwepo.

Kwa kawaida , taifa hilo lilikabiliwa na tatizo la mafuriko kwa mwezi Agosti na septemba.

Je, mzozo huu unaweza kupelekea mapigano?

Image caption

Mvuvi wa ziwa Nile, Ethiopia

Kumekuwa na hofu kuwa mataifa haya yanaweza kuingia katika vita kama watashindwa kupata suluhu ya mzozo wao.

Mwaka 2013, kulikuwa na ripoti za siri zinaoonyesha kuwa wanasiasa wa Misri wanapendekeza kuwepo kwa mapigano dhidi ya Ethiopia ili kupinga ujenzi wa bwawa hilo.

Rais Sisi alinukuliwa pia akisema kuwa Misri itatumia mbinu zote kulinda haki zake katika mto Nile.

Mwezi uliopita waziri mkuu wa Ethiopia aliwaambia wabunge kuwa hakuna nguvu inayoweza kutumika kusitisha ujenzi wa bwawa hilo.

Mwaka jana, Kundi la kimataifa la usuluhishi walitoa angalizo kuwa nchi hizo zinaweza kujiingiza katika vita kwa sababu ya mzozo wa ujenzi wa bwawa.

Marekani kuingilia kati suala hilo inaonyesha uhalisia wa ugumu wa suala hilo na kuna uhitaji wa kukabiliana na mzozo huo.

Misri inadhani kuwa Marekani kuingilia kati mzozo huo kutaleta athari kubwa baada ya rais Sisi kumuomba rais Trump kuingilia kati mgogoro huo ambao Ethiopia hawakuwa tayari kukubaliana nao.

Mgogoro wa mataifa hayo mawili ambayo ni washirika wa Marekani, wameibua mzozo huo ambao unadhaniwa kuwaweka mamilioni ya watu hatarini.

Nini kinatarajiwa?

Hatua inayofuata itakuwa mawaziri wa maji wa nchi zote mbili pamoja na waziri wa mambo ya nje kujaribu kuafikiana na maridhiano yanayotaiwa Januari 15.

Siku ya mwisho hiyo iliwekwa mwezi Novemba baada ya wawakilishi wa pande zote mbili walipokutana Marekani.

Mkutano wa aina hiyo unatarajiwa tena kufanyika hivi karibuni mjini Washington.

“Suala hili linahitaji makubaliano ya nchi zote tatu.” Waziri wa maji wa Ethiopia aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha
US president’s office

Image caption

Donald Trump akiwa na wawakilishi wakuu wa Misri, Ethiopia na Sudan katika Ikulu ya Marekani 6 Novemba, 2019

Kama wakishindwa kufikia maafikiano Januari 15, wawakilishi hao wanaweza kuomba msuluhishi mpya kufikia makubaliano yaliojadiliwa Novemba mwaka jana.

“Kile ambacho kinahitajika kutoka kwetu ni kuwakilisha ripoti kwa viongozi wetu kwa sababu viongozi wetu wanaweza kuwa na utaratibu wa kutatua tatizo hili ,” bwana Seleshi alisema.

Siku ya jumapili, waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitaka rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa kusaidia kutatua mgogoro huo.

Bwana Abiy alisema kuwa kiongozi ajae wa Umoja wa Afrika bwana Ramaphosa anaweza kutatua tatizo hilo kwa amani.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *