Mzozo wa Mto Nile: Je, mzozo wa Ethiopia, Misri na Sudani kuishia wapi?


Bwawa la Reinnesance nchini Ethiopia linapingwa na Misri na Sudani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Bwawa la kufua umeme la Reinnacence nchini Ethiopia limezaa mgogoro baina ya nchi hiyo na Misri na Sudani.

Jaribio la rais wa DR Congo na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Felix Tshisekedi kuzipatanisha nchi za Misri, Sudan na Ethiopia kuhusu mzozo wa mto Nile limefeli siku ya Jumatano na kurejesha nyuma kabisa jitahada za kupata mwafaka kuhusu jinsi mataifa hayo yatavyomaliza malumbano ya kutumia maji ya Nile .

Ethiopia imjenga Bwa kubwa litakalotegemea mto Nile ili kuzalisha kawi na kuendeleza kilimo lakini Misri inasema bwawa hilo linahatarisha kiwango cha maji kitakachofika Misri nan chi jirani ya Sudan.

Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi anasema kuwa Misri inaheshimu hamu ya Ethiopia ya kujiendeleza kupitia maji yake ya Mto Nile, mradi masilahi ya maji ya Misri hayatatizwi.

El Sisi hata hivyo anaishtumu Ethiopia kwa kujaribu kupendekeza jambo ambalo haliwezekani kwa kusimama kidete kwamba lazima itajaza bwawa lake hilo na ahajachelea kuashiria kwamba Misri iko tayari kuchukua hatua yoyote kuyalinda maslahi yake – hatua inayoashiria uwezekano wa nchi hizo kujipata katika mgogoro wa kivita kuhusu maji ya Nile.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *