Netflix: Yajipata mashakani kwa tafsiri mbaya ya maandishi ya kiswahili katika video zake


Picha yenye tafsiri ya maandishi ya kiswahili katika kanda za video za Netflix

Haki miliki ya picha
Photo/courtesy

Image caption

Picha yenye tafsiri ya maandishi ya kiswahili katika kanda za video za Netflix

Mahitaji ya lugha ya kiswahili yameongezeka duniani huku baadhi ya vyuo vikuu vikianzisha lugha hiyo pamoja na vitivo kamili.

Sekta ya burudani pia haikuwachwa nyuma katika kutumia Kiswahili hususan kupitia kutafsiri kazi zao kwa lugha hiyo ili kuwalenga takriban watu milioni 200 wanaoizungumza.

Ni kutokana na lengo hilo ambapo kampuni ya burudani ya mitandaoni duniani Netflix imeanzisha maandishi ya tafsiri ya Kiswahili katika kanda za video katika Runinga na filamu zake.

Lakini siku chache tu baada ya kuzindua tafsiri hiyo katika kanda zake za video, wateja wanaolengwa wamekosoa tafsiri hizo wakisema kuwa ni kiswahili kibovu.

Maandishi hayo ya tafsiri sio sahihi na mengine yana ucheshi hatua iliowafanya watu mitandaoni kuitaka kampuni hiyo kuimarisha tafsiri yao.

Netflix ina zaidi ya wanachama milioni 148 kati zaidi ya mataifa 190, wanaotazama vipindi vyake katika runinga pamoja na makala kupitia lugha tofauti

Wanachama wanaweza kutazama chochote wanachotaka wakati wowote, na mahala popote katika skrini yoyote mtandaoni.

Pia wanaweza kucheza, kusitisha kuendelea kutazama bila ya kuingiliwa na matangazo katikati.

Haki miliki ya picha
Reuters

Mmoja wa waliokashifu tafsiri hiyo mbaya kwa Jina Thinguri alisema, Nipatieni ajira , naweza kufanya kazi nzuri katika tafsiri yenu zaidi ya munavyofanya.

Mwengine kwa jina Kenan alisema: Hii tafsiri katika Netflix haina tatizo. Mwisho wa siku Netflix ni mtandao wa burudani na maandishi ya tafsiri hiyo yanaburudisha.

Wengi walilalamikia kuhusu tafsiri ya maandishi hayo yenye ucheshi.

”Mungu wangu tafsiri ya maandishi: Your Highness -urefu wako. Je ni Waganda waliotafsiri?” alihoji mmoja ya watumiaji wa mtando wa Twitter.

Mwengine kwa jina Patrick aliongezea: Lazima kuna Mkenya ambaye aliwashauri Netflix kuweka tafsiri hiyo ya maandishi ya kiswahili katika kanda zao za video ili kuvutia wateja wake wengi , Cha kushangaza ni vipi aliweza kufika katika ofisi zao na kazi kama hiyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *