Ni kwanini watoto wachanga hutelekezwa mpakani mwa Rwanda na DRC?


Watoto hawa wamekuwa wakiachwa katika sehemu chafu na hatari kwa afya zao na pasipo mtu wa kuwahudumia

Image caption

Watoto hawa wamekuwa wakiachwa na mama zao katika sehemu chafu na hatari kwa afya zao na pasipo mtu wa kuwahudumia

Idadi kubwa ya watoto wachanga ambao wamekuwa wakitelekezwa na mama zao wanaovuka mpaka kuingia katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo(DRC) wamepatiwa hifadhi.

Serikali ya Rwanda imeamua kujenga kituo maalumu cha kuhudumia watoto hao.

Mwandishi wa BBC mjini Kigali anasema watoto hao wamekuwa wakiachwa katika sehemu chafu na hatari kwa afya zao na pasipo mtu wa kuwahudumia.

Mpaka baina ya Rwanda na Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, unaofahamika sana kama ‘petite bariere’, ni eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara ndogondogo na kubwa, huku mamia ya watu kutoka Rwanda na DRC wakivuka mpaka kila siku hususan kwa shughuli za biashara.

Wanawake ambao wengi ni wafanyabiashara wa biashara ndogo ndogo mara nyingi huambatana na watoto wao wachanga wanapovuka mpaka kutoka na kuingia Rwanda.

Eneo moja lililojaa taka na Nzi katika mji wa Rubavu uliopo upande wa Rwanda limekuwa ni eneo ambalo wamekuwa wakitumia kuwatelekeza watoto wao wachanga wakati wakienda Kongo kwa ajili ya biashara zao ndogo ndogo.

Hii ndio sanbabu iliyosababisha serikali kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la ADEPE kuanzisha kituo cha kuhudumia watoto hao,kituo kinachoitwa ‘Petite Bariere’

”Mpakani nilikuwa namuacha mtoto huyu mchanga na dadake, lakini baadae dada yake alilazimika kuacha shule ili kumlea mdogo wake, Sasa hapa wanatusaidia kwa ushauri wa uzazi wa mpango na pia kutupatia mikopo ya kuendeleza mashirika yetu ya kujiendeleza ”, amesema Bi Joselyne Umuhoza, mmoja wa akina mama ambao waliwaleta watoto wao kwenye kituo cha malezi ya watoto wanaotelekezwa.

Image caption

Kituo cha malezi ya watoto wachanga wanaotelekezwa cha Petite Barriere kina watoto zaidi ya 20

Hadi sasa kituo cha malezi ya watoto wachanga wanaotelekezwa kina watoto zaidi ya 20, ambao huhudumiwa kwa kupewa uji, na huduma nyingine zikiwemo za kiafya

“Hapa mtoto anaweza kupata uji, chakula cha mchana na kuwa na muda wa kupumzika. Watoto hawa wana daktari ambaye huwafwatilia kila siku. Tunafanya kazi pia kwa karibu na vituo vya afya katika kitongoji chetu kuhakikisha watoto wanatunzwa na kuhudumiwa kwa hali ya kibinadamu”, anasema Louise Mukeshimana ni mratibu wa kituo.

Tunawatunza watoto wa kati ya miezi saba na miaka mitatu, na kuchochea akili zao ili waweze kukua vizuri , aliongeza Bi Mukeshimana.

Matunzo ya watoto kwenye kituo cha watoto cha ‘Petite Bariere’ hutunzwa toka Jumatatu hadi Jumamosi, ambapo wazazi huacha watoto wao na kuja kuwachukua jioni , ili kuwaleta tena siku inayofwata.

Image caption

Lango la kituo cha malezi ya watoto wachanga wanaotelekezwa

”Mtoto wangu nilimleta katika kituo hiki .Alipokelewa vizuri, anapata huduma zote. .Walipomchukua alikuwa na miezi 7 na atatimiza umri wa miaka 3 hivi karibuni. Hapa pia wanatusaidia kwa ushauri wa uzazi wa mpango na pia kutupatia mikopo ya kuendeleza mashirika yetu ya kujiendeleza” Anasema Mukarukundo Gaudance mmoja wa akina mama wafanyabiashara wadogo wadogo mjini Bukavu.

Huduma ya malezi ya watoto wachanga wanaotelekezwa na mama zao wanaofanya biashara ndogo ndogo hutulewa bure.

Kituo kina uwezo wa kuwachukua watoto 80 tu huku wanaotimiza miaka 3 wakiwa wanapelekwa katika kituo kingine chenye shule za bure.

Unaweza pia kusikiliza:

Huwezi kusikiliza tena

Watoto wenye ulemavu wa ngozi walia ukiwa

Vituo vingine zaidi ya 4 kama hiki vimejengwa pia katika sehemu zingine za Rwanda.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *