Ni miaka 30 tangu kuanguka ukuta wa Berlin


Shamrashamra za maadhimisho ya miaka 30 ya tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin zimeanza kote nchini Ujerumani. Rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anawaalika wakuu wenzake kutoka mataifa ya Poland, Slovakia, Jamhuri ya watu wa Czech pamoja na Hungary huko mjini Berlin.

Kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin mnamo Novemba 9 mwaka 1989 kulifuatia uasi wa amani kwenye iliyokuwa Ujerumani Mashariki baada ya kuimarika kwa vuguvuvu miongoni mwa mataifa ya Ulaya yaliyokuwa kwenye eneo linalodhibitiwa na uliokuwa muungano wa kisovieti, walioamua kzigeuzia mgongo siasa za Moscow.

30 Jahre Mauerfall Berlin (Reuters/F. Bensch)

Kansela Angela Merkel amesema kuna uwezekano wa mcgakato wa muungano kukamilika baada ya miaka 50

Karibu matukio 200 yamefanyika katika kipindi cha wiki moja iliyopita ikiwa ni pamoja na kuoneshwa kwa vidio ya wakati maelfu ya raia wa Ujerumani mashariki walipouvunja ukuta huo uliokuwa na urefu wa kilometa 155 ili kuingia upande wa magharibi.

Kansela Angela Merkel wanatarajiwa hii leo kuhudhuria kumbukumbu maalum kwenye makumbusho ya ukuta huo wa Berlin. Alipozungumza na gazeti la Ujerumani la Süddeutsche, Merkel amesema huenda mchakato wa muungano kati ya Magharibi na Mashariki ukachukua hata miaka 50 hadi kukamilika.

“Katika masuala kadhaa, ambako inaaminiwa kwamba kila kitu kinaweza kufanana kati ya Mashariki na Magharibi, hii leo tunashuhudia kwamba inaweza kuchukua nusu muongo ama zaidi” aliliambia gazeti hilo la Süddeutsche.

Mapema hii leo rais Steinmeier kupitia tovuti yake aliwaalika raia wa Ujerumani kusimulia shuhuda zao  binafsi za kuanguka kwa ukuta huo wa Berlin.

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *