Nigeria: Kwa nini wahalifu wa kimtandao ni 'mfano wa kuigwa'?


Uhalifu wa Kimtandao

Haki miliki ya picha
Getty Images

Katika mfululizo wa barua kutoka waandishi wa Afrika, Mtaalam wa riwaya wa Nigeria Adaobi Tricia Nwaubani anadai kuwa kwamba matapeli wa mtandao wamekuwa mfano wa kuigwa na vijana wengi katika nchi yake..

Hivi karibuni Shirika la upelelezi la Marekani (FBI) liliwafungulia mashtaka watu 80 miongoni mwao raia 77 wa Nigeria ambao imewataja kuwa ”mtandao mkubwa wa wahalifu wa kimtandao katika historia ya Marekani”.

Lakini kilichowagutusha raia wengi wa Nigeria ni kukamtwa kwa mfanyibiashara mashuhuri wa kimataifa, Obinwanne Okeke.

Mkuu huyo wa shirika laNigeria la Invictus Group, ambalo linajihusisha na biashara katika sekta ya kilimo na ujenzi wa nyumbaaliwahi kutajwa na jarida la Forbes mwaka 2016 kama mmoja wa wafanyibiashara wakubwa barani Afrika walio na umri wa miaka chini ya 30

Sasa Bw. Okeke – au Invictus Obi kama anavyofahamika na wengi – anatuhumiwa na mamlaka nchini Marekani kwa wizi wa dola milioni 11 (£8m) kupitia uhalifu wa kimtandao.

Amekanusha mashtaka dhidi yake alipofikishwa mahakamani wiki iliopita na kuzuiliwa rumande.

Shirika la upelelezi la Marekani, FBI limekua likitoa orodha ya wahalifu kila baada ya miaka kadhaa na mamlaka husika huwafungulia mashtaka watuhimwa na baadhi ya wale wanapatikana na hatia kufungwa jela.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Nigeria ina idadi kubwa ya watumiaji wa simu aina ya smartphone barani Afrika

Lakini hatua hiyo haijawazuia wanaume raia wa Nigeria kujiunga na mtandao wa wahalifu wa kimtandao duniani

Wanigeria walipopata sifa ya uhalifu wa kimataifa mara ya kwanza katika miaka ya 1990 kwa kuwaibia raia wa mataifa ya ulaya mamilioni ya dola katika kashfa zilijulikana kama 419.

Siku hizi uhalifu huo amabo unajulkikana kama Yahoo Yahoo hutekelezwa mtandaoni kupitia barua pepe na programu tumishi za ujumbe.

Mara nyingi huwa utapeli wa kimapenzi au kibiashara ambao ajenti maalum wa FBI Michael Nail wakati mmoja aliufananisha na ” uporaji wa kisasa wa benki”.

“Unaweza kukaa nyumbani ukiwa umevalia nguo za kulala na kutumia kompyuta na kuibia benki bila silaha,” alisema.

Ushauri wa kiusalama mtandaoni

Haki miliki ya picha
Getty Images

  • Wahalifu wanajihusisha na utapeli wa kimapenzi mtandaoni kwa kuchunguza na kukusanya taarifa za watu mtandaoni kwa kutumia vigezo kama mtindo wamaisha na utajiri ili kuwarubuni wahasiriwa wao.
  • Polise wanaweza kusaidia kwa uchunguzi na kuwachukulia hatua wahalifu hao lakini ni vigumu kupata pesa zilizopotea.
  • Wahalifu Huficha mienendo yao kwa kutumia anuani yao mtandaoni au kwa kutumia nambari za simu ambazo hazijasajiliwa.
  • Usitume pesa kwa mtu usiyemjua mtandaoni.
  • Tafakari madhara ya kuweka taarifa binafsi mtandaoni -huenda ikatumiwa na wahalifu kukutapeli.

Chanzo: Kitengo cha polisi cha Uingereza cha kukabiliana na uhalifu

Kundi la kwanza la wahalifu wa kimtandao wa Nigeria waliofahamika kama 419 hawakua na elimu ya kutosha.

Kundi la pili linahusisha vijana wadogo na watu walio na elimu ya juu ambao hawana ajira kutokana na uchumi wa mbaya uliosababishwa na utawala wa kiimla wa kijeshi uliochangia usimamizi mbaya wa raslimali ya umma.

Mara nyingi wanawaona wahalifu wasiokuwa na ajira wakijilimbikizia mali na kuamua kujiunga nao.

Na kundi la tatu ni lile linalovutiwa na ujasiri wa wahalifu hao ambao wanauwezo wa kuiba kwa urahisi mamilioni ya madola kutoka kwa wanasayansi wa Marekani, wakurugenzi wa Uingereza na wanazuoni wa Ujerumani.

Chuo cha mafunzo kuvamiwa

Walichanganua jinsi wahalifu walivyobuni biashara halali kwa njia ya kidanganyifu kutokana na fedha zilizopatikana kwa njia ya udanganyifu na hatimae kuwa wahisani wakubwa au wanasiasa walio na ushawishi mkubwa katika jamii.

Watu kama hawa wanawachocheo watu kuiga mfano wao na vijana wengi nchini Nigeria wanachukulia uhalifu wa kimtandao kama moja ya njia ya kujipatia ajira na chanzo cha mapato.

Mwezi Mei mwaka huu, Shirika la Nigeria la kupambana na uhalifu wa kiuchumi,lilivamia” chuo cha mafunzo cha Yahoo Yahoo”katika mji wa kibiashara wa Lagos, na kumtia nguvuni msimamizi wa chuo hicho na wanafunzi wanane waliodai kufunzwa mbinu ya kutekeleza uhalifu wa kimtandao.

Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI lilipotangaza kuwa limebaini kuwa mfanyibiashara mashuhuri wa Nigeria alikuwa akijiuhusisha na uhalifu wa kimtandao taifa hilo liligutushwa na hatua hiyo huku baadhi ya watu wakielezea jinsi alivyowaaibisha.

Vyombo vya habari viliangazi amtindo wa maisha wa mfanyibiashara huyo anaefahamika kama Obinwanne Okeke na wenzake, Lakini suala hilo halikujadiliwa kwa muda mrefu kwa sababu baadhi ya watu walihoji kuwa mfanyibiashara huyo na wenzake hawana hatia hadi mahakama itakapowatia hatiani.

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kijamii wamependekeza njia kadhaa za kuwashauri vijana nchini humo kujiepusha na mienendo ya kutaka kujitajirisha kwa njia za mkato.

Kanda ya video ya washukiwa hao wakionesha utajiri wao kwa kuandaa hafla za kifahari zilisambazwa mitandaoni, ambapo wageni waalikwa wanasakata densi juu ya sakafu iliyojaa madola na ‘kuogelea’ vinywaji vya bei ghali.

Haki miliki ya picha
EFCC/FBI

Image caption

Mamlaka nchini Nigeria na Marekani zimekua zikikabiliana na Uhalifu wa Kimtandao

Pia picha zilizosambazwa mitandaoni zinawaonesha washukiwa hao wakijumuika na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali.

Mtu mmoja ambaye yuko katika orodha ya FBI ya wahalifu alikua katika kamati iliyoandaa sherehe ya kutawazwa kwa gavana mpya miezi mitatu iliyopita.

BBC hata hivyo haijathibitisha uhalisia wa video na picha hizo.

Maafisa hao wa serikali walikanusha kuwa na uhusiano wa karibu na washukiwa hao.

Lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine walaghai ni watu tunaowafahamu vizuri.

Huenda ni ni ndugu zetu, ‘marafiki wa ”marafiki zetu” au, jamaa zetu wa karibu.”

”Mtu mmoja ambaye amekuwa katika orodha ya FBI ya wahalifu sugu kwa miaka kadhaa hatimae alipatikana na hatia ya wizi wa dola milioni 40 mwaka 2013, ni mwana wa pekee wa rafiki ya mama yangu wa karibu niliyemfahamu tangu utotoni mwangu tukiwa mjini Umuahia kusini mashariki mwa Nigeria,” anasema Adaobi Tricia Nwaubani mwandishi wa vitabu wa Nigeria

Ikiwa atapatikana na hatia Bw. Mr Okeke anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 30 jela, wanasema wataalamu. Kesi yake itaendelea kusikizwa mwezi Februari mwaka 2020.

Raia wa Nigeria wanahofia huenda uhalifu huo huenda ukawanyima fursa wafanyibiashara halali wa nchi hiyo kutambuliwa kimataifa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *