Njia mpya ya kukabiliana na uwindaji haramu Afrika


A uniformed dog handler with her springer spaniel at Jomo Kenyatta International Airport in Nairobi, Kenya

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Wawindaji haramu barani Afrika ambao walikuwa wakisakwa na kila aina ya silaha na hata helkopta, sasa wameanza kusakwa kwa mbwa anayetumia pua yake kufichua uhalifu au waalifu.

Mbwa hao maalum wapatao 50 wamepelekwa katika mataifa sita ya Afrika kwa ajili kuibua wawindaji haramu.

Mbwa hao wana uwezo wa kunusa na kubaini pembe za ndovu, tembo na sehemu za wanyama wengine , waliweza kupelekea mamia ya wawindaji haramu kukamatwa na hata njia ambazo huwa wanazitumia kuweza kujulikana.

A springer spaniel on a conveyor belt at Jomo Kenyatta International Airport looking at the hand of a handler - Nairobi, Kenya

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Tangu taasisi ya wanyapori Afrika (African Wildlife Foundation) kuanzishwa mwaka 2011, sehemu za wanyamapori zapatazo 400 ziliweza kukamatwa tangu programu hiyo ianze.

Mkurugenzi wa mbwa hao wa uhifadhi wa wanyama pori bwana Will Powell, alisema kuwa ushirikiano huo wa serikali na sekta binafsi umeweza kusaidia ufanisi wa mbwa hao.

“Hii inajumuisha mikakati sahihi ya namna ya kuabiliana na changamoto hii ya uharamia. Hivyo kwa msaada wa serikali, tuliweza kuwafundisha askari wa porini namna ya kufanya kazi na mbwa ambao wana uwezo wa kunusa na kubaini uhalifu.”

Two dog handlers with their dogs at Jomo Kenyatta International Airport, outside the DHL warehouse, in Nairobi, Kenya

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Mbwa hawa walipelekwa kafanya kazi na wafanyakazi wa mamlaka ya wanyamapori wa Tanzania, Kenya, Uganda, Msumbiji, Botswana na hivi karibuni walipelekwa Cameroon.

Walinzi wa wanyama pori walipewa mafunzo kwa muda wa wiki 8 mpaka 10.

Askari wa wanyama pori walihusishwa na mbwa hao wa kunusa kama wenza wao katika kazi, ingawa awali askari hao walikuwa hawajazoea kufanya kazi na mbwa hapo awali, wao walikuwa wanajua kuwa mbwa huwa kazi yao kulinda tu.

A group of trainee dog handlers sitting on the ground and patting a dog on a lead in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Walijifunza kuwapenda, kuwajali na kuwaheshimu mbwa wao.

“Mbwa ambao wamepelekwa Cameroon hivi karibuni wamedaiwa kuwa na macho kama wanataka kulia”, kwa mujibu wa

bwana Powell.

A springer spaniel on a conveyor belt at Jomo Kenyatta International Airport sniffing luggage - Nairobi, Kenya

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Bwana Powell aliwachagua mbwa hao kutoka Ulaya, katika mataifa ambayo yamezoea utamaduni wa kufanya kazi na mbwa kama Netherlands, Czech Republic na Hungary.

Mbwa hao walikuwa wamepatiwa mafunzo tayari na kufananisha kiwango cha elimu yao sawa na kuwa na shahada ya uzamivu.

“Huwa tunatafuta mbw ambao ni werevu ili iwe rahisi kuwapa maelezo na kuwasafirisha,” alisema bwana Powell, raia wa Uingereza ambaye alianza kazi ya kuwafundisha mbwa kunusa katika maeneo ya migodini.

A Malinois dog with its ears pricked to attention in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

“Lazima wawe marafiki ili waweze kufanya kazi na mtu yeyote aliyepata mafunzo ya kufanya kazi na mbwa.”

Kuna aina mbili ya mbwa wa aina hii ambao ni ‘Malinois na springer spaniels’.

Malinois, asili yao ni Belgian wanasifika kwa kuwa werevu, wakali na wanaweza kukabiliana na hali ya joto.

A Malinois dog running during training in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Huku ‘springer spaniels’ wana pua nzuri na huwa wana asili ya urafiki .

Bwana Powell alieleza.

Two springer spaniels running during training in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

“Huwa ni kawaida watu kuogopa mbwa, lakini katika mazingira ambayo unapaswa kufanya kazi na mbwa kila mara ni vyema kutumia mbwa aina ya ‘spaniels’.”

Mbwa aina zote mbili wana uwezo wa kufanya kazi vizuri kabisa kwa sababu wanapenda kushughulika kila wakati.

A springer spaniel on a conveyor belt at Jomo Kenyatta International Airport sniffing luggage - Nairobi, Kenya

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Maisha ya kazi kwa mbwa huwa inategemea na kizazi chake.

Kwa upande wao ‘Malinois’, wanaweza kufanya kazi kwa miaka 12 au 13 .

Huwezi kusikiliza tena

Fahamu kwa nini mbwa huyu anatumia kiti cha kutembelea

Wakati ambapo muda wake wa kufanya kazi unapoisha huwa wanatafuta makazi katika nyumba za watu wa karibu au wanarudishwa kwa bwana Powellanayeishi Tanzania.

“Tulianza kuwafundisha mbwa kunusa pembe za ndovu ambazo huwa ni ngumu kuzinusa na huwa zinatoroshwa kiurahisi,” alisema.

“Sasa hivi tunawafundisha kunusa mfupa wa wa simba na meno yake ambayo huwa yanasafirishwa nchini China kwa ajili ya kutengeneza dawa.”

A Malinois dog on a lead sniffing blocks during training in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Kuwafundisha mbwa kunaweza kuchukua miezi mitano.

Vitu vyote ambavyo vinatengenezwa na sehemu za wanyama pori wana uwezo wa kuvipata hata kama vilifichwa sana.

A springer spaniel on a lead walking past luggage, which has laid out on the grass, during training in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Wanapofanya kazi hiyo mbwa huwa wanapata pembe za ndovu au tembo zikiwa na harufu ya kahawa au pilipili zikiwa zimefunikwa na mfuko wa plastiki.

Wameweza pia kubaini meno ya simba ambayo yalikuwa yamefichwa katika chupa ya chai.

Mbwa wanavyobaini kitu huwa wanazawadiwa mdoli kwa kufanya kazi nzuri.

Will Powell holds a Malinois dog by a lead as it walks past luggage laid out on the grass during training in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Mbwa waliofundishwa kunusa mizigo ya bidhaa za uhalifu katika mipaka au vyombo vya usafirishaji .

Mbwa hao wanafanyakazi katika uwanja wa ndege wa kimataifa, katika mataifa ya Afrika Mashariki na hata katika mamlaka za bandari ya Mombasa na Dar es Salam.

Short presentational grey line

Unaweza kuvutiwa kusoma taarifa hizi pia:

Short presentational grey line

Mbwa huwa wanasababisha wasafirishaji haramu kutumia gharama kubwa kufanikiwa na uhalifu wao na hata kutumia njia hatari zaidi.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta l, Nairobi,Kenya eneo ambalo bidhaa 51 za wanyama pori zilikamatwa zikisafirishwa kinyume na sheria katika mwaka mmoja. Mwaka 2019 idadi iliweza kufanikiwa.

A springer spaniel walking over boxes at a warehouse in Jomo Kenyatta International Airport with a handler by their side - Nairobi, Kenya

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

“Wasafirishaji bidhaa hizo kwa njia ya haramu walijua tupo. Na matokeo yake kilo 23 ya pembe za ndovu zilikamatwa Uganda,” alisema bwana Powell.

“Mtu huyo alinunua ndovu Nairobi lakini alijua kuwa kuna mbwa hivyo akaamua kwenda ba basi mpaka Entebbe, lakini alikamatwa huko.”

Kila eneo kuna changamoto chake na mikakati yake. Kwa mfano Msumbiji katika uwanja wa Maputo, walinzi wana tabia ya kusalimia wasafiri wanapoweka mizigo yao kwa ukaguzi.

Will Powell, with a dog sitting on a table, talking to trainees during a session in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Presentational white space

Mbwa wote huwa wanalishwa biskuti zilizotolewa kwa ufadhili wa kampuni ya Ufaransa,Royal Canin, ambayo inaunga mkono programu hiyo .

Na mbwa wote wanaishi katika bustani au eneo la mapumziko.

A trainee dog handler lounging on the grass and playing with a dog in Arusha, Tanzania

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Serikali inaheshimu utaratibu wao unaojulikana kama ‘Five Freedom’.

Kila mbwa wa kunusa ameajiriwa na taasisi ya ‘ African Wildlife Foundation’.

“Ushirikiano wa askari sio na mbwa ila zaidi ya mbwa,” alisema bwana Powell.

Mafanikio ya programu hii hutegemea askari na serikali husika katika jitihada za kukabiliana na uwindaji haramu na usafirishaji wa bidhaa za wanyamapori.

“Kile tunachotaka kukifanya ni kusitisha biashara hii haramu.”

A dog handler holding the lead of a black dog that is sniffing containers at Jomo Kenyatta International Airport in Nairobi, Kenya

Haki miliki ya picha
Paul Joynson-Hicks

Picha zote zina haki milikiSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *